6:06 AM
Wakati nikiwa naishi kwa furaha,majivuno
ya nchi yangu nzuri yenye utajiri na amani yakutosha na pia kuweza
kupambanua mambo ilikua ni mwanzoni mwa miaka ya 80 niliona watu
wakiishi kwa ujamaa maana ilikua jambo la kawaida sana kwenda kula au
hata kulala kwa jirani bila wasi wasi; na maisha yalikua burudani
sana kwakua tulikua tukiombana moto,chumvi,unga,mafuta ya kupikia,ya
taa na hata machanuo kwaajili ya kuchana nywele.
Wakati huu
sikuwahi kusikia mtu kaua au kuuwawa na mtanzania mwenzake ila sasa
ndio imekua kurasa za mbele za magazeti kama tulivyokua tukiona
kutoka kwa nchi za wenzetu,Tulikua tukimwona Baba wa Taifa hili akiwa
kavalia kaunda suti na fimbo mkononi na akipita kila kona ya nchi
tukiwa tunaimba ule wimbo wa Taaaaanzania tanzaniaaaa nchi yenye
....... na ikifika saa12jioni kila mtu anatii amri ya kushusha
bembera yetu nzuri.
Mwishoni mwa miaka ya 80 na mwanzoni mwa miaka
ya 90 tulikua tukitumie zile noti zetu zenye ubora na picha mbali
mbali za mali asili ya Tanzania na tukiwasiliana kwa barua(s.l.p),
nilikua nikiona wakubwa zangu wakipendana na kujumuika pamoja kwenye
sherehe mbali mbali kama EID,KRISMAS,KOMUNIO NA KIPAIMARA! Na wakati
huo ukisikia siasa utamsikia Cleopa Msuya, Agustino Lyatonga Mrema,
John Momose Cheyo nk.
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 nikiwa Sekondari
tukiwa chini ya Mzee wetu Mkapa kiongozi aliekua Imara na mwenye
maamuzi magumu na yenye kusimamisha jamii kwenye mstari sahihi,
tulianza kuingia rasmi kwenye teknolojia mpaka viganjani.Suala la
bara bara ya shauri moyo lilileta mtafaruku kidogo baada wa wanadini
kukataa barabara isipite makaburini.
Ila kiongozi imara akazungumza
na kazi ikafanyika na leo tunafurahia bara bara ile na Machinga
complex imejengwa pale.
Mwishoni mwa miaka ya 2000 tukiwa na MH
RAIS J M KIKWETE, Nchi yangu ninayoipenda kwa dhati ikiwa chini ya
vyama vingi nikiwa na imani kwamba ndio tunasonga mbele na kuendelea
kupeperusha bendera ya Amani na Upendo Duniani, gafla bendera ile
ikaanza kwenda kinyume na mwelekeo wa upepo wa Amani yetu.
NAKUMBUKA
VYEMA MH KAKA YANGU NINAEMWESHIMU SANA ZITTO KABWE alichangia maada
ya Wizara ya katiba na sheria kuhusiana na mjadala wa mahakama ya
Kadhi hapa tz na akasema, nanukuu "tz ni nchi inayoheshimu dini
zote na haifungamani na upande wowote ila wanasiasa wetu
wanapandikiza utofauti wa kidini ambao ni sumu kali itakayo angamiza
vizazi vyetu'
Ndugu zangu maneno ya Mh ZItto ni mazito sana na
ukiyachambua kifalsafa utapata maana kubwa na kuona kua alikua
akilenga mbele na si kwa wakati ule, wakati haya yakisema na mh, kuna
wengine walikua wakibeza na kusema wapinzani hawana jipya wanatafuta
sympath kutoka kwa wananchi.
Leo hii naandika maneno haya ni
mwanzoni mwa mwaka 2013 nchi yangu ninayoipenda na nitakayokufa
nikiitumikia na inayomlea mwanangu ipo katika CHUKI,FITNA NA MAUAJI
YA KIDINI ambayo yanahitaji kiongozi mwenye nguvu na uchungu na nchi
hii kuyamaliza kwa kutumia fimbo yake ya uongozi na vyombo vya sheria
kama alivyofanya mkapa wakati wa Shauri moyo.
Kiini cha dini
yoyote ni kuimarisha Amani na kueneza utulivu na upendo miongoni mwa
waumini wake na si kueneza njia za kulipiza kisasi endapo kuna
aliekukosea kwa kua kusamehe ndio misingi ya dini zetu.
Malumbano
yanayoendelea ya kidini na chuki zitakazoangamiza vizazi vyetu ni
yakukomeshwa kwakua bado tuna nanafasi na watanzania ni wasikivu na
waelewa sana.
Niwakati umefika tujue kua hawa wanasiasa na
viongozi wa dini wanaochochea vuruga hii leo, vurugu hizo zikianza
watakua wakwanza kukimbiza familia zao na sisi ndio tutakaobaki
kuumia na kuuana, kama kuna ambae amefika kwa jirani zetu
Kenya,Uganda na Rwanda ataelewa ninachosema.
Maadhara ya vurugu za
kidini ni kuuana,kuchukiana,kutosaidiana na mbaya zaidi kubaguana kwa
itikadi za dini! Je, ni watanzania wangapi wameoana au kuzaa na mtu
asie na dini kama yake? je vurugu hizi zikiendelea wale watoto
tutawaua? kama tutawaua je wanahatia yoyote? Je, tumefikia hatua
yakwenda kinyume na maandiko ya vitabu vyetu vya dini?
Je imefika
hatua kile chombo na watu wake yaani wabunge na mawaziri tuliokua
tukiwaogopa, kwa heshma na hadhi zao katika Taifa letu kutukana
hadharani; tena mbele ya kiongozi mkubwa kama Spika wa Jamhuri ya
muungano? Kile kinachoendelea bungeni kwa sasa ni machungu ya uonevu
wa kisiasa na maslahi ya vyama badala ya mustakabali wa Taifa letu
linalomegwa kila kukicha na hawa hawa viongozi wetu.
Mzee PIUS MSEKWA
na SAMWELI SITTA ni viongozi wakujivunia katika nchi hii
kwakuliongoza vyema bunge letu bila kujali itikadi za chama
walichotoka ila walitambua fika kua wapo katika kiti kwa manufaa ya
Taifa hili lililojaa wapuuzi kama hao wanaoporomosha matusi na
mabishano binafsi ndani ya Bunge Tukufu(ingawa naona hata aibu
kuliita Bunge Tukufu kwa haya yanayofanyika ndani yake)
Kama kweli
Tanzania tumeingia vyama vingi basi tafadhali Baba mwambie Mama
mwenye nyumba awape wapinzani nafasi watoe yaliyomo vinywani
mwao(Mama yangu aliwahi kuniambia BORA MATAPISHI KULIKO UOZO TUMBONI}
waacheni waseme au wabwabwaje kama msemavyo kuliko kuwapandikiza
chuki miyoyoni mwao.
Kabla ya hitimisho niseme kwamba tuwe sana
makini na hizi social media zetu maana ni rahisi sana kusambaza
mawazo hasi na asie mwerevu ni rahisi kufuata alichosoma na
kukifanyia kazi.
Ndugu zangu nchi hii haiongozwi na Muislam wala
Mkristo bali inaongozwa na mtanzania aliechaguliwa na watanzania wote
yaani WAKRISTO,WAPAGANI NA WAISLAM.
MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU
WABARIKI VIONGOZI WANGU NA UWAPE WEREVU WAKUWEKA TAIFA MBELE KATIKA
MAJUKUMU YAO NA MAMBO YA BUSARA.
Ni mimi mtanzania mwenzako
Basil
Komu(Bazo)
0 comments:
Post a Comment