Wednesday, March 27, 2013

ZITTO KABWE APINGA KAULI YA KUUWAWA ILIYOANDIKWA NA GAZETI LA MTANZANIA LEO.



Haya ni mambo manne aliyosema Mbunge wa Kigoma ZITTO KABWE juu ya gazeti la Mtanzania la leo lililoandika Habari SIRI YA KUUWAWA ZITTO YAFICHUKA

1.   Mtanzania leo imeandika habari 'Siri ya kuuwawa Zitto yafichuka'. Habari hii sio ya kweli. Sijawahi kukutana na Ben Saanane hata siku moja

2.   Siamini kabisa kwamba Katibu Mkuu CHADEMA anaweza panga kuniuwa mie. Hana sababu kufanya hivyo.

3.   Pia sijawahi kufika na wala siijui Hotel ya Lunch Time Mabibo. Ninaomba Mtanzania wathibitishe na vyanzo vyao habari hiyo


4.   Siwezi kukaa kimya nionapo uwongo unasemwa hata kama uwongo huo ulilenga, labda kunisaidia. UWONGO ni UWONGO tu.

0 comments:

Post a Comment