Friday, March 22, 2013

TUNAAZIMISHA SIKU YA MAJI BILA MAFANIKIO KATIKA MAJI

JOHN MNYIKA

Mbunge wa ubungo mh john mnyika amesema tanzania hatuna haja ya kusherekea siku ya maji bali ametaka au ametoa rai kwa serikali kuitumia siku hii kutatua matatizo ya maji.

“unawezaje kusherekea siku ya maji wakati una matatizo ya maji mimi naona siku hii ingetumika kutatua matatizo tuliyonayo kuliko kusherekea jambo ambalo linatusumbua”

vile vile Mnyika amesema watendaji wa serikali hawana uwezo wa kutenda na kumtetea Raisi kama walivyo dhaminiwa na kupewa nafasi za utendaji  kutokana na kitendo cha baadhi ya viongozi katika Wizara na Mamlaka za maji kushindwa  kujibu maswali waliyoulizwa na Raisi kutokana na ukosefu wa maji katika jimbo la Ubungo ,Dar es salaam  na Nchi kiujumla.

Mnyika aliendelea kusema kuwa baadhi ya viongozi katika Wizara na Mamlaka za maji wamegeuza mradi kwa kuhujumu rasilimali hiyo kwa masirahi yao binafsii


0 comments:

Post a Comment