Friday, March 22, 2013

J MARTIN'S, AY NA MWANA FA NDANI YA NGOMA MOJA

AY

Msanii J  Martin kutokea Nigeria na Aliekuwa pruducer wa Psguare  Mwanzo Amefanya kazi na Wasanii wakali wa Tanzania AY pamoja na FA  katika studio za MJ RECORDS chini ya produza MARCO CHALII.

Katika wimbo huo J Martin amefanya vesi nzima na kafanya hivyo kutokana na ukweli kwamba alipenda kazi hiyo japo wahusika mwazo walifikili kumpa nafasi ya chorus tu lakini baada ya kuisikia ngoma na kuvutiwa  nayo alijikuta akitaka kufanya vesi nzima .

Ngoma hiyo kwa mujibu wa mwana FA Inatarajiwa kutoka mwishoni mwa mwezi wa nne au mwanzoni mwa mwezi wa tano japo amesema kuwa mwezi wa nne wanategemea kufanya Video ya ngoma hiyo ili kuwaonesha watanzania kile walichoimba katika ngoma hiyo.

0 comments:

Post a Comment