Friday, March 22, 2013

DULAYO KUJA NA FACEBOOK

DULAYO

Msanii wa Bongo fleva Dulayo anataka kuachia tracck yake mpya inayokwenda kwa jina la SUBIRA lakini kwa mujibu wa stori iliyopo ndani baadhi ya watu walioisikia track hiyo wameibatiza jina la Facebook.

Ndani ya subira A.K.A Facebook Dulayo amezungumzia juu ya msichana aliekutana kutokana na mitandao ya kijamaa kama facebook anasema kuwa ilikuwa vigumu kwa binti kumuelewa kwa kuwa tu walikuwa hawajawahi kuonana hivyo alihisi labda alikuwa akitaniwa au  alitaka kuchezewa.

Lakini baadae walikuwa kitu kimoja mpaka kufikia hatuwa ya kuwa Mume na mke hivyo sasa Mtu mzima Dulayo anamkumbusha mkewe kuwa unakumbuka tulipokuwa tukichat na kuwasiliana kupitia mitandao ya kijamii,tulikuwa hatufikili kuoana lakini mpaka imefikia kuwa wapenzi.

Hiyo ndio facebook ya dulayo swali sasa jeeeeee? KUNA UHALISIA KATIKA HALI HII UNAWEZA FUNGUKA YAKO KWA UZOEFU WAKO NA HII MITANDAO YA KIJAMIIII. 

0 comments:

Post a Comment