YANGA inapenda kutoa angalizo kuwa tabia hiyo iliyokithiri ni
ukiukwaji wa Sheria na unaikosesha Klabu mapato halali ambayo ingeyapata
kutokana na matumizi ya Nembo yake.
![]() |
| Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Lawrence Mwalusako (kulia) akiongea na waandishi habari makao makuu ya klabu leo, kushoto ni Baraka Kizuguto Afisa Mawasilano wa klabu ya Yanga |
Kwa
mantiki hiyo, kuanzia leo hii, YANGA inatangaza rasmi kuwa ni marufuku kwa
kampuni, mtu binafsi au kikundi chochote kutengeneza ama kuuza bidhaa
zenye nembo ya YANGA bila ridhaa ya Klabu ya YANGA. Iwapo itatokea mtu yoyote
kukiuka taarifa hii, basi YANGA itachukua hatua kali za kisheria ili kukomesha
tabia hii mbaya ya KINYONYAJI.
Klabu ya
Yanga imepata taarifa kuwa kuna baadhi ya wafanyabishara na watu mbalimbali
ambao wanajihusisha na utengenezaji wa bidhaa zenye nembo ya YANGA ambao
wanakusudia kuingiza bidhaa mbalimbali nchini zenye nembo ya YANGA kwa nia ya
kuziuza.
YANGA
inatoa tahadhari kuwa kitendo hicho ni uvunjaji wa sheria na matumizi yasiyo
halali ya nembo yake na yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua kali za
kisheria.
YANGA
inawashauri wale wote wanaotaka kuingiza bidhaa au kuuza bidhaa zenye nembo
yake wawasiliane na uongozi wa Klabu ili waweze kuingia makubaliano rasmi kwa
yule ambaye atakubaliwa kuingiza bidhaa hizo zikiwa ni zenye kiwango na ubora
ambao utakubaliwa na kupitishwa na YANGA.
Mtu
yeyote mwenye nia hiyo basi awasiliane na KATIBU MKUU wa Klabu Ndugu LAWRENCE
MWALUSAKO katika Makao Makuu ya Klabu Mtaa wa TWIGA/JANGWANI, Dar es Salaam.
MWISHO
kabisa, YANGA inatoa wito kwa wanachama na wapenzi wake kutonunua bidhaa zozote
zenye nembo ya YANGA Iwapo muuzaji huyo hajaruhusiwa rasmi na YANGA kwani tabia
hiyo inaikosesha KLABU mapato na kuifanya kuendelea kuwa tegemezi.
Imetolewa
Dar es Salaam tarehe 22 March 2013.
LAWRENCE
MWALUSAKO







0 comments:
Post a Comment