Monday, April 13, 2015

Mpenzi wangu hakupendezwa picha yangu na Nay wa Mitego-Dayna Nyange

Na Gerald Kitalima

NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva Dayna Nyange ambae anauwakilisha mkoa wa Morogoro katika tasnia ya muziki amefunguka na kusema kuwa picha alizopiga na Nay wa Mitego zimemkwaza mpenzi wake,Dayna alisema haya alipokuwa
akihojiwa katika kipindi kimoja cha Radio (XXL cha Clouds Fm).
Mwanamuziki huyo ambaye kwa sasa ameachia wimbo mpya unaofahamika kama 'Nitulize' anasema kuwa picha hizo zenye utata machoni kwa watu zilipigwa kwa ajiri ya kutengeneza Cover ya wimbo huo mpya lakini anadai kuwa alivaa nguo za kuogea ndiyo maana katika picha hizo ameonekana kama hajavaa nguo yoyote juu.



Ni kweli picha hizi zimenipa shida na kunifanya kugombana na mpenzi wangu lakini nashukuru baadaye aliweza kunielewa,unajua sikuwa na lengo la kupiga picha ya namna hii lakini mpiga picha wetu ndiye alitoa wazo hilo hivyo Nay wa Mitego alibidi apige kivua wazi na mimi nilikuwa nimevaa nguo ya kuogea,hivyo mikanda ya nguo ya kuogea ilizibwa na nywele zangu ndiyo maana haionekani na watu wanadhani nilipiga nikiwa sina nguo"



"Lakini nilivaa nguo sema ilikuwa ni nguo ya kuogea sema kwa kuwa picha ile ilikatwa kuanzia kiunoni kuja juu inamfanya mtu ajue kuwe huenda tulikuwa falagha na kuhisi labda hatukuwa na nguo lakini mimi nilikuwa na nguo na Nay wa Mitego pia alikuwa na nguo" Aliongeza Dyana.



Mbali na hilo Dyana alielezea tetesi zilizopo kuwa huenda anatoka na msanii Roma Mkatoliki na kusema kuwa yeye hana mahusiano ya kimapenzi na Roma ila tu Roma amekuwa mtu wake wa karibu sana ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika kazi zake za sanaa na hata katika maisha ya kawaida kuwa wamekuwa wakishauriana mambo mengi.
"Unajua Roma Mkatoliki ni mshikaji wangu kitambo sana yaani nipo nae karibu ila sina mahusiano naye ya kimapenzi,tumekuwa tukishauriana na kuelimishana mambo mbalimbali kuhusu maisha hata sanaa yetu,hivyo naweza kusema Roma anamchango mkubwa katika kazi yangu ya sanaa"



Akielezea kuhusu sanaa yake Dyana alisema anaamini muda ukifika ataweza kufahamika na kufanya vizuri kama wasaniii wengine ila kwa sasa hawezi kufanya kazi na wasanii wa nje kama ambavyo wasanii wengine hufanya.



"Ni kweli mimi nimeanza muda muziki na nimekuwa nikijitahidi kufanya kazi nzuri na kutoa video nzuri lakini siwezi kulalamika kwanini siwi msanii mkubwa kihivyo kama wengine ila naamini kuwa muda ukifika kila kitu kitakuwa sawa,maana siwezi kufanya muziki wa kiki ili nitambulike kila kona ila muda ukifika nitakuwa msanii mkubwa kama wengine tu."



























0 comments:

Post a Comment