Tuesday, March 10, 2015

HASIRA ZA MASHABIKI ZINANIPA NGUVU-RAMA DEE

Na Gerald Kitalima
Rama Dee amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook alipodai kuwa mashabiki na upungufu wa muziki wa RnB Tanzania ndicho kilichomsukuma
kufanya kazi hiyo.

"Kikubwa nilichokifanya kwenye hii nyimbo mpya ya USIHOFIE WACHAGA, Ni hasira za mapungufu ya ladha za RnB zilizokuwa chini hapa Nyumbani.Bado najifunza mengi na kufunza wengi pia.Fans wangu wananipa hasira sana,na nitazidi kufanya kwa faida yenu siku zote."

Kazi mpya ya Rama dee imetengenezwa na ELY DA BWAY ndie produza alie tengeneza ile ngoma "Kama HuweZi" Mkali huyu yupo pale Ubungo (Home Town studio) mbali na ngoma hii alitengeneza kazi mwisho ya Rama Dee akiwa na Lady Jaydee ambayo ilitoka mwaka jana na kufanya vizuri sana katika vituo mbalimbali.

Baada ya kuachia kazi hiyo baadhi ya mashabiki wa Rama Dee walikuwa na haya ya kusema juu ya kazi hiyo ambayo mpaka sasa toka imetoka inasiku tatu na kusikika masikioni mwa watanzania walio wengi kupitia mitandao ya kijamii na vipenid mbalimbali vya Radio.

"RJ Mkali: Mimi kwakweli nimeisikia na nimeshaipata kupitia mitandao ya kijamii.Niseme kweli braza we ni noma bado sijaona zaidi yako usipotee sana kaka huwa tunakosa vitu kama hivyo"

"Erick Mlelwa: Mimi nimeipata na nimesikiliza ila kikubwa nimegundua sauti yako ni ya kipekee sana all in all we need your vocol all the time

"Dullahkagoda Daaah ..Wewe jamaa unajua sana RnB nasema hivi wimbo huu utaishi zaidi ya miaka 100 ..Ama hakika upendo hauchagui kabila/humu duniani wabaya wamewazidi wazuri Ahsante Rama Dee kwa radha ya masikio."

Kufuataia mapokezi mazuri ya mashabiki wa Rama Dee katika wimbo huu ndio unamfanya Rama Dee kuona bado anadeni kubwa kwa mashabiki wake ambao wanaonyesha kukosa ladha ya muziki ambao yeye anaufanya ndio maana amesema kuwa mashabiki wake wanazidi kumpa hasira ya kufanya kazi nzuri siku zote.



0 comments:

Post a Comment