Sunday, February 8, 2015

SIWEZI KUMUOMBA MSAMAHA-LADY JAYDEE

Na Gerald Kitalima
Msanii nguli wa bongo Fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee amefunguka na kuweka wazi kuwa katika maisha yake ya
kawaida,maisha ya sanaa na maisha ya utafutaji amekuwa akikutana na changamoto mbalimbali zinazopelekea muda mwingine mpka watu kugombana au kutofautiana kutokana na mtazamo au matatizo mbalimbali na amedai wazi kuwa katika watu wote ambao aligombana nao na yeye kugundua ndiye alikuwa chanzo cha ugomvi huo wote alishawaomba msamaha na wanaendelea na maisha ya kila siku.Lady Jaydee alisema hayo jana kupitia ukurasa wake wa Instragram wakatia akijibu maswali 10 yaliyotokana na maswali kibao kutoka kwa mashabiki wake.



"Nitapatana na mtu atakae kubali kuwa alikosa, km naamini yeye ndio alinikosea itabidi aniombe msamaha.Kama mimi ndio nilikosa nitaomba pia msamaha Otherwise hakuna miujiza Siwezi kumuomba mtu msamaha endapo naamini kabisa sijakosa .Niliowahi kuwakosea nilishawaomba msamaha wooote.Hakuna binadamu asie kosea ila siwezi ku surrender kiuongo au kwa uoga wa maisha.Naamini hata nikiuza nyanya bado wapo watu wanaohitaji nyanya, na watanunua."



baadhi ya mashabiki waliuliza kwanini Lady Jaydee hana ushirikiano na wasanii wenzake wa kike katika muziki na yeye aliweka wazi kuwa amekuwa akishirikiana nao sana tu mpaka kufikia hatua wengine kuwatungia wimbo,Jide anadai kuwa mara nyingi ili msanii aweze kutoka au kufanya vizuri lazima kazi zake zipate promo ya kutosha katika vituo mbalimbali vya Redio na bahati mbaya yeye sio mwenye hizo redio.



Nimewahi kufanya na wasanii mbali mbali wa kike ila sijui kwanini hamjaziskia.
1.Mwasiti amewahi kunishirikiisha
2. Nimewahi kumuandikia na kushiriki kuimba kwenye wimbo wa movements za Albino na Kaysha
3. Nimewahi kumwandikia na kushiriki kuimba nae Nakaaya Sumari
4. Nimewahi kumwandikia wimbo Patricia Hillary
5. Nimewahi kumshirikisha RAY C kwenye wimbo wangu toka Album ya Machozi unaitwa, Nimekubali na wapo wasichana mbali mbali waliopita Machozi Band na kujifunza kuimba leo mnawafahamu,Kumbukeni tu kuwa kutoka kwa mtu itategemea na nyimbo zake kuwa promoted redioni na mimi sio mwenye hizo redio.Msaada pekee ni kushiriki kila ntakapotakiwa kufanya hivyo"



Lady Jaydee kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Forever ambao amemshirikisha mdogo wake anaefahamika kama Dabo na pia mwanadada huyo amepanga kufunguka mengine mengi ambayo nayo tutakuletea kupitia www.eatv.tv

0 comments:

Post a Comment