Sunday, February 8, 2015

DOGO JANJA AFUNGUKA YA MOYONI

Na Gerald Kitalima
Msanii Dogo Janja ambae kwa sasa amerudi chini ya uongozi wake wa zamani amefunguka ya moyoni na kusema kuwa katika kipindi
kirefu watu wamekuwa wakimzungumzia vibaya na kumsema kuwa amepotea katika muziki wa Bongo,Dogo Janja amefunguka hayo leo baada ya jana kuweza kufanya show kali katika viwanja vya Mwananyamala na kupokewa vizuri na mashabiki wake ambao walionyesha kumkubali Janjaro.



"Wapo Waliosema Janja Aliotea/Janja Kapotea/Janja Ameanguka HaweZi Simama Akatembea/ Mtaani Maneno Kibao,Mpaka kwenye Mitandao ya kijamii Watu Wanakusema Utadhani Unakula Kwao..!Hii ilikua Jana Viwanja Vya Mwananyamala Uzinduzi Wa............ Mungu Akubariki Father Madee Ali Mungu Akutie Nguvu Tuzidi Kusonga NP: Janjaro Bado Yupo Kama Desturi Na Mila."



Mwanamuziki Madee Ali kutoka Tip Top Connection siku za karibuni alipokuwa katika kipindi cha The Cruise ya East Africa Radio alisema kuwa wakati wa Dogo janja kurudi katika game umefika na muda wowote kuanzia sasa ataachia wimbo wake mpya ambao nao ushakamilika.



Dogo Janja alikuwa chini ya usimamizi wa Madee kabla ya kushindwana na kutimukia katika kundi la Mtanashati Entertainment lililokuwa chini ya uongozi wa Ostadhi Juma na Musoma lakini hata hivyo kundi hilo liliweza kutamba kwa muda na kupotea huku Dogo Janja nyota yake ikionekana kupotea ndipo alipoona haja ya kurudi kwa baba yake mlezi ambae alimfunza muziki na kumsimamia katika maisha ya kila siku Madee Ali.



0 comments:

Post a Comment