Tuesday, February 24, 2015

GK ATANGAZA KURUDI RASMI JUMATATU NA VANESSA MDEE

Na Gerald Kitalima



Msanii ambae pia ni kiongozi wa kundi la East Coast Team GK amesema sasa ni wakati sahihi kwake kurudi
katika muziki na kufanya kazi ya muziki baada ya kumalizana na masuala ya shule,GK ambae anatarajia kuachia kazi yake 
mpya siku ya Jumatatu ambayo amemshirikisha msanii Vanessa Mdee na kazi hiyo imetayarishwa na produza mkongwe John Mahundi na Markochali.


King Crazy GK alidai kuwa John Mahundi ilibidi asafiri kutoka Marekani na kuja bongo kufanya kazi hiyo ambayo anaamini watanzania watampokea na kumuelewa baada ya kimya cha muda mrefu,Mkali huyo mwenye miondoko ya michano amedai kuwa kazi hiyo ambayo itatoka siku ya Jumatatu imesimamiwa na msanii Ay.


"Kama unavyotuona hapa mapishi yameshakamilika na watanzania wakae tayari kwa kazi nzuri kutoka kwangu nikiwa na Vanessa Mdee,naamini mashabiki zangu wananisubiri na mimi nasema kwa sasa siwezi kuwaangusha kabisa,maana kama masomo yamekwisha kwa sasa ni kazi tu na wategemee mambo mengi kutoka kwangu na kutoka kwa East Coast Team nzima"


Msanii King Crazy GK kwa mara ya mwisho alitoa wimbo wake wa mwisho uliokuwa na maadhi ya Kwaito ambao alifanya na Yuzo na wimbo huo ulifahamika kama Baraka au laana? ambao haukufanya vizuri sana katika vyombo mbalimbali vya habari.

0 comments:

Post a Comment