Na Gerald Kitalima
Mwanamuziki anaetamba na hits single ya Akadumba Nay
wa Mitego amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake ya
utafutaji
na kuhangaika na sanaa kuna watu wengi waliamini kuwa anapoteza muda.
Nay amesema watu hao pia wanadai kuwa bangi ndizo
zinampotezana kufanya muziki ambao waliamini kuwa unaleta chuki au
usingeweza kumtoa na kumtabulisha kama wasanii wengine ambao
walitamba kipindi hicho yeye akitafuta kutoka.
Nay wa Mitego alisema kuwa katika kuhangaika na
muziki ilifika mahali hata mzazi wake ambaye ni mama yake mzazi
alimfukuza nyumbani kwake akiwa darasa la saba sababu ya muziki ambao
leo umeweza kumfungulia njia na kumpa mafanikio ambayo hata mzazi
huenda anayafurahia.
"Wakati Naanza kila mtu aliniona kama napoteza
muda hivi, wengine walisema bangi ndo zinanipoteza. Ata mama mzazi
alinifukuza nyumbani nikiwa darasa la Saba sababu ya huu Muziki ninao
ufanya sasa."
Mbali na kukatishwa tamaa Ney anadai kuwa hakuweza
kukata tamaa sababu alikuwa anatambua nini anakifanya hivyo alizidi
kukomaa na kuona kuwa anafikia malengo yake ya kufanikiwa kupitia
muziki wa Bongo Fleva na kupata heshima hata kwa watu ambao walikuwa
wanaona anapoteza muda.
"Sijawahi kukata tamaa nikiamini siku moja
nitakuja kufanikiwa na wataniheshimu wote wanaonidharau..Thnx God kwa
kunipa moyo wa ujasiri mpaka nilipo Leo..!! Angalau naheshimika,
nackilizwa..Wengi wao leo wanajivunia Ney-Wamitego"
Mkali huyo kupitia ukurasa wake wa Instragram
amewataka vijana kutokata tamaa na wazidi kutafuta pesa kwani hata
yeye moja ya ndoto yake ni kuona anaishi maisha ya kitajiri na
anaamini yatatimia hivi karibuni.
"Washkaji zangu eeh!?? Tutafuteni #Hela tuacheni
masihara kabisaa.Kiukweli mimi napenda kuishi maisha mazuri
yakitajiri (like a boss) na nina imani nitaishi ivyo soon, coz
nikikumbuka nilikotoka daah..!!! Huwa sometimes siamini kama ni Mimi
(Ahsante Muziki_Media_Mashabiki).
0 comments:
Post a Comment