Thursday, January 29, 2015

MAHUSIANO YA MAPENZI SI KIKI-TIMBULO

Na Gerald Kitalima
Mwanamuziki anayetamba na single yake ya Nakumiss miss, Timbulo amefunguka na kuweka wazi kuwa katika maisha yake ya
muziki hategemei mahusiano yake ya kimahaba kuwa 'Kiki' ya kazi yake ya muziki anayofanya.



Timbulo amesema kuwa anaamini katika kufanya kazi nzuri na kuiacha kazi yake isimame yenyewe ndiyo maana hawezi kupeleka mambo yake ya mahusiano katika vyombo vya habari.

Timbulo amefunguka hayo katika ile programu yake ya kuweka wazi historia ya maisha yake kupitia katika mitandao yake ya jamii.
Timbulo anadai katika maisha yake ya mahaba amepitia mambo mengi lakini hayupo tayari kuweka wazi mambo hayo na huo ndio utaratibu aliojiwekea.

Katika simulizi hiyo mkali huyo anadai kuwa katika kupenda ilifika mahali mpaka baadhi ya watu walimwambia kuwa ana moyo wa kike ingawa mwanzo hakuweza kuwaelewa watu hao lakini kadri siku zinavyozidi kwenda anakiri kuwa hivyo.

"Niliwahi kuambiwa nina moyo wa kike, ni kitu ambacho mwanzo sikukielewa lakini siku hadi siku nimekuwa nakisadiki, ni vile mimi sio msemaji na siamini kama mahusiano yangu ni kiki ya kazi yangu ndiyo maana huwa si entertain sana mahusiano yangu kwenye vyombo vya habari nauacha muziki wangu usimame wenyewe."

Timbulo anadai katika maisha yake ya mahaba anaogopa sana kipindi cha kuachwa lakini anakili kuwa katika kipindi hicho ndiyo huwa anakuwa na hisia kali za kuandika nyimbo nzuri na ndiyo huwa anafanya nyimbo nyingi zaidi akiwa katika hali ya kuachwa kwa kuwa huwa anakuwa na hisia na katika nyimbo ambazo aliandika katika hali hiyo zote zimefanya vizuri zilipotoka na kupokelewa vyema na mashabiki wake.

"Nathubutu kusema najua sana kupenda na huwa naogopa sana zile scene (part) za kuachana asikwambie mtu ni moja kati ya nyakati ngumu sana kwenye maisha yangu japo ndiyo wakati ambao huwa nafanyaga nyimbo nyingi na ofcoz nyingi zimefanya vizur so naamin ndio wakati ambao huwaga naandika nyimbo nzuri sana maana huwaga ndo faraja yangu, ......kumpenda mtu huwaga ni dakika kumsahau sasa ndo kizungumkuti"

Kabla ya kutamba na Nakumiss miss Timbulo alishawahi kutamba na nyimbo nyingine ikiwemo Domo Langu Zito, Sina Makosa, waleo wakesho na nyinginezo.



0 comments:

Post a Comment