Thursday, January 29, 2015

NUHU HAWEZI KUNIPIGA HATA NIKIMKOROFISHA-SHILOLE

Na Gerald Kitalima
Msanii na mwigizaji Zuwena Mohammed Shilole maarufu kama Shishi Baby amefunguka na kuweka wazi kuwa mpenzi wake Nuhu
Mziwanda huwa hawezi hata kurusha ngumi ili hali yeye huwa anamkolofisha.




Shishi amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instragram baada ya kupatana na mchumba wake huyo ambaye weekend hii waligombana na kutofautiana.
Shishi Baby ambaye ni mama wa watoto wawili anadai kuwa Nuhu Mziwanda ndiye mwanaume sahihi kwake maana huwa hawezi hata kumpiga hata kama yeye ndiye kafanya makosa, anakili wazi kuwa yeye ndiye amekuwa jeuri katika mahusiano yao lakini Nuhu huwa ajali hilo kwani anamvumilia na ndiyo maana baada ya hapo wanapatana na maisha yanaendelea kama kawaida na hiyo yote anadai ni kwa kuwa wanapendana.
"Huyu Nuhu mjanja wangu mimi. daah nimekamatika hapa na naamini ni mwanaume sahihi kwangu maana hawezagi kurusha hata ngumi japo namchokozaga, mie mjeuri tu. mnaomuandama mume wangu mmeshindwa. kugombana ni kawaida sana kwenye mapenzi na kama niliwaudhi mashabiki wangu mnisamehe mmi nampenda mume wangu."
Lakini mashabiki mbalimbali wa Shilole wanaonesha kutofurahishwa na kitendo alichofanya juzi cha kugombana na Nuhu Mziwanda tena mbele za watu na kusema kuwa kufanya hivyo ni kumdhalilisha na kujidhalilisha wenyewe.
Renrishikweli:- @shilolekiuno utafanya wanaume wawaogope wadada wenye pesa...then huyo Nuhu ni pesa tu hana, siku akipata atakumbuka unavyomdhalilisha atakimbia kama mwanariadha..kama unampenda mpe heshima yake iwe ndani ama nje....labda kama ni kiki ila kama ni kweli, sio vizuri.
Juliuss100Yan:- unampiga makofi mbele za watu Nuhu ndio ukome kuoa wazee ..**tusi***... wewe
Bakarihemed5Km:- Unampenda kweli mpe heshima yake lakini wewe ufanyi poa kwake why ulifanya vile juzi?.
ShangaineemaDah:- Kweli we lijali Nimekukubali safi sana. Mwanaume Huyu siku akiamua hana mjadala @shilolekiuno hongera sana yaani Wapo wachache sana kama @mziwandanation so be carefully. Ujaribu kujicontrol hasira, Nuhu anawazazi, ndugu na mashabiki kwahiyo kumbuka wanampenda Nuhu hivyo chochote utakachofanya kidogo au kikubwa kitayumbisha uhusiano.Tusingependa yatokee mabaya. Inshaallah Allah awape subira, uvumilivu na hekima ili Muoane.
Hayo ni baadhi ya mawazo ya mashabiki wa Shilole kufuatia ugomvi wao wa majuzi ambao ulitokea na kushuhudiwa na watu katika tamasha la KibokoYao ambao ulipelekea watu hao kuwa tofauti kwa siku mbili na baadaye kuamua kumaliza tofauti zao ili waendelee na maisha yao ya kila siku.
Nuhu Mziwanda na Shilole ni wapenzi kwa muda sasa na mwishoni mwa mwaka jana walivalishana pete ya uchumba.



0 comments:

Post a Comment