Thursday, January 29, 2015

MAPRODUZA HARUHARIBU BONGO FLEVA-MESEN SELEKTA

Na Gerald Kitalima
Msaani na mtayarishaji wa muziki wa bongo fleva Mesen Selekta amedai kuwa watayarishaji wa muziki wa Tanzania hawajaharibu
muziki wa bongo fleva kama ambavyo watu wamekuwa wakitupia lawama na baadhi ya mashabiki.




amesema kuwa watu wamekuwa wakidai kuwa watayarishaji hao wamekuwa wa kwanza kubadili bongo fleva na kukopi midundo ya muziki wa ki Nigeria na Afrika Kusini.
Mensen amesema hilo leo alipokuwa akihojiwa na watangazaji wa kipindi cha Power Jams ya East Africa Radio Sam Misago na Anna Peter.
Mensen alidai kuwa watanzania hatuna muziki wetu ambao unaweza kututambulisha kama ilivyo kwa wenzetu hivyo wasanii wengi wanafanya kazi kwa kufuata upepo wa muziki kwa kipindi hicho, ndio maana wanamuziki wengi wa bongo wanahitaji kufanya kazi ambazo zinakuwa na midundo ya 'kinaijaa' kwa sababu tu ndiyo muziki unaofanya vizuri kwa sasa.
"Siwezi kusema kuwa maproduza ndiyo tunaharibu muziki wetu sababu hatuna identity katika muziki, ndiyo maana wasanii wetu wanafanya kazi kwa kufuata upepo wa muziki wakiona muziki wa Nigeria upo juu na wao wanatamba kufanya kama wa Nigeria wakiona watu wa Afrika Kusini wapo juu na wao wanafanya kama watu wa Afrika Kusini"
Kwa upande wake Mtayarishaji Monagansta ambaye ametengeneza 'hits song' kibao ikiwemo Vitamin Music ya Belle 9 na Dear Gambe ya Young Killer na nyingine kibao, amesema kuwa kitendo cha muziki wa bongo sasa kuwa kama wa Nigeria au wa Afrika Kusini unasababishwa zaidi na msanii mwenyewe ingawa hata maprodyuza nao wanachangia.
"Ni kweli kwa sasa kumekuwa na midundo mingi ya Nigeria na Afrika Kusini katika muziki wetu lakini hii yote inasababishwa na vitu viwili kwanza hatuna muziki wetu ambao tunaweza kujivunia nao, lakini pili wasanii wenyewe, kwani unaweza wewe mtayarishaji ukawa umetengeneza midundo fulani na wasanii wakija kusikiliza kazi zako unakuta wanahitaji midundo ambayo ndani yake iwe na vionjo vya Nigeria au Afrika kusini"
Mbali na hilo Monagansta alisema yeye kama mtayarishaji anafanya muziki kama biashara na wateja wake ni wasanii hivyo kama wasanii wao wanataka midundo yenye vionjo vya Nigeria au Afrika Kusini hana budi kufanya hivyo ili mwisho wa siku aweze kufanya biashara ndio maana inafika mahali muziki wetu unakuwa na vionjo vya Nigeria na Afrika kusini.



0 comments:

Post a Comment