Mwanamuziki
Prof Jay ambae kwa sasa anafanya kazi yake ya muziki huku
akijihusisha na biashara mbalimbali ikiwemo Saloon na biashara ya
muziki kupitia
katika studio yake ya Mwanalizombe,Prof ameonesha wazi
kuwa kuna haja kubwa kwa wanafunzi kusoma sana wanapopata nafasi hiyo
ili kuja kukabiliana na maisha mbele ya safari.
Mwanamuziki
huyo amejaribu kutoa mfano kwa kuonesha aina ya maisha ambayo alikuwa
akiishi kipindi ambacho alikuwa shuleni ambapo ameonesha hakuwa
makini sana na Elimu kitu ambacho kwa sasa anakijutia na kutamani
angepata nafasi toka enzi za kutambua aina ya maisha atakayokutana
nayo.
“Darasa
la tano 'b'. ... Daftari moja masomo yote.. Tungejua yanayokuja
kutokea huko mbele...Tungesoma mpaka tupate KIBIYONGO... #ELIMU
KWANZA!!”
Hili
liko wazi kwa viajana wengi tunapenda kupuuza Elimu na kuona kama
kitu kisocho na msaada kwetu na kuhitaji maisha fulani ya haraka
hali8 ambayo baadae huwa tunakuja kuijutia kwa namna moja au nyingine
pindi tuonapao wenzetu ambao waliweza kuvumilia na kumshilikia Elimu
jinsi ambavyo mambo yao wanakuwa wakiyaendesha.
Kwa
kuliona hili tunapaswa kushirikilia Elimu na kuifanya kuwa kitu cha
kwanza huku tukisubili mambo mengine ambayo yatakuja baada ya Elimu.








0 comments:
Post a Comment