Friday, February 7, 2014

KIMYA CHA ROMA CHAWATESA MASHABIKI WAKE

Mashabiki wa msanii Roma Mkatoliki ambae amejiwekea utaratibu wa kutoa wimbo mmoja kwa mwaka mzima na kutegemea wimbo huo huo kumuweka katika ramani ya muziki wa Hip Hop hapa Bongo wameonesha hali ya kushindwa kuvumilia ukimya wa Ninja na kumtaka atoe ngoma mpya.
Kwa mwaka jana msanii Roma aliachia wimbo wake wa 2030 na toka hapo watu wamekuwa na kiu ya kutaka kusikia ngoma mpya kutoka kwa Ninja Roma Mkatoliki.

Katika kumbukumbu zangu msanii huyu mwaka jana Tarehe 28 ya mwezi 11 alitoa ahadi ya kuachia wimbo mpya siku 12.12.2013 akiwa anasherekea miaka kadhaa ya kuzaliwa lakini cha ajabu haikuwa hivyo na hakutoa taarifa yoyote tena juu ya kuachia kwa ngoma hiyo ambayo alianza kuidokeza na mistari kama hii Ukikosa shukrani kama kimbunga, utaishia kugongea weed/ Kama ustaadh anayengoja mpunga au maandazi ya maulid/ Rooooma!! 12/12/2013!!.

Kwa watu ambao tumekuwa tukimfuatilia msanii huyu tuliingia na wasiwasi kidogo kwani kile alichoaahidi hakikuwa hivyo na akipiga kimya kutokana na suala langu la kutaka kujua ukweli ilinibidi nimcheki Ninja mwenyewe kujua nini kimetokea mzigo umeshindwa kutoka katika siku aliyoahidi,na majibu yalikuwa kuwa kuna mipango imeingiliana na kuharibu mpangilio wa hiyo ngoma na kushindwa kutoka katika hiyo siku aliyoahidi.

Kwa akili ya haraka haraka ikanituma kuwa kila mwaka unapoisha ndipo msanii huyu anatoa wimbo kwani hata 2030 ilitoka mwezi wa 12 wa mwaka 2012 ingawa kwa mipango yake pia alikuwa amepanga wimbo huo kutoka katika siku yake ya kuzaliwa lakini ilishindikana siku hiyo ila baada ya siku kadhaa ilitoka.

Imekuwa tofauti sana na wimbo huu wa sasa ambao alianza kutupa vionjo vya mistari yake kwani mwezi wa 12,1 na sasa tupo mwezi wa 2 Ninja bado hajafanya mambo hivyo anaibua maswali mengi kwa mashabiki zake ambao wengine wameanza kumuhitaji atoe ngoma hiyo kwani amekuwa kimya kwa muda mrefu sana,mwenyewe najiuliza mengi kwamba nini kimemtisha kutoa wimbo huo mwanzoni kabisaa mwa mwaka?Je kuna kitu anahofia juu ya muziki wake?au ni maamuzi tu kwa kuwa anaona ananafasi ya kuweza kurudi vizuri katika game?



Mussa Selemani bro, nakukubali sana mimi shabiki wa muziki wako wa kwanza then kala jereiah but unatisha nakukubali sana. mimi niko lushoto tanga



Abuu Kombo Baba Wabongo ndivyo walivyo, Mimi naamin nafasi yako na fikra zako hakuna wakuweza kukufata wala kukukaribia "jipange



Barack Jacks Mkigoma Tupe kitu kaka... We need ya New HIT 
 
Zuberi Zayumba Zbwaa ROMA@amini usiamini fanc wanaham na new song from u mpka imepitiliza achia kaka usijeukashangaa hata ku2kanwa wa2 wanamamzuka achia bana watoto wanasumbua

Joyce John Mkaya tatizo watu wanafikiri Hip Hop inatungwa ka Bongo flavor Hip hop inahitaji muda me nakuaminia Roma Tongwe



Johmafa Real #EfeEfraim Akaunt h n ya roma pamoja naya R.O.M.A na group lake n Ongea na Roma hana akaunt nyngne zaid ya hz.af pia mzwaze mafans wa roma yupo kwenye kiota anasuka bonge la ngoma hajaw toa ngoma kal hyo mwez hu wa 3/4 inapress rasm mta kwa mtaa uvumilivu tu



Tselemuca Mkangara inachelewa banaaaaa Eroooo!!



UJUMBE WANGU KWAKO ROMA
Hawa ni baadhi ya mashabiki wako Roma ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisubili muziki wako kwa kuwa bado wanamahitaji na wewe na wanahitaji muziki wako so huu ndio muda muafaka kwako kuwapa kile wanachotaka,najua unatambua wazi kuwa kila moyo unamwisho wake katika kusubili jambo itafika wakati hawa watu ambao wanakuhitaji hawatakuwa na hitaji na wewe wala muziki wako kwa kuwa watakuwa wameshajenga mapenzi na mwanamuziki mwigine au muziki mwigine.

Hali hii ndiyo inawasumbua wasanii wengi wa Bongo ambo kwa sasa tunasema ni wakongwe katika Game na bado wao wanahitaji kufanya muziki lakini jamii haiwapokei kama ambavyo awali walikuwa wakipokelewa,maana unaweza kuwa ni msanii mzuri kwa kuwa tu nina amini wewe ni mkali lakini nikipata nafasi ya kumsikiliza mwingine huenda akawa vizuri kuliko wewe sema sikupata nafasi ya kumsikiliza na kumuelewa lakini kwakuwa umenipa nafsi hiyo nikagundua hilo hivyo wewe hautaweza kunirudisha nyuma kwa kuwa naweza kupata kitu kizuri zaidi upande wa pili.












0 comments:

Post a Comment