Raia
wa Ugiriki, Alexandria Athanasios (30), amekamatwa kwa tuhuma za
kukutwa na kilo 5.3 za dawa za kulevya aina ya heroine katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es
Salaam.Meneja Usalama wa uwanja huo, Clemence Jingu, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba raia huyo wa kigeni alikamatwa juzi saa 3:00 usiku uwanjani hapo.
Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Nzowa, akifafanua zaidi tukio hilo alisema Athanasios alikamatwa wakati akijiandaa kusafiri na ndege ya shirika la Swiss Air kutoka Dar es Salaam kwenda Ugiriki kupitia Zurich.
0 comments:
Post a Comment