Baada
ya kupokea barua yake ya mashtaka 11 tarehe 01/12/2013 ambayo
anashitakiwa nayo na iliyomtaka ajitetee kwa maandishi,Mheshimiwa
Zitto Zuberi Kabwe (MB) jana tarehe 10/12/2013 amefanya hivyo kwa
mujibu wa Katiba na
Kanuni za Uendeshaji za Chama
Pia
Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe (MB) ametoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa
Chama kumueleza nia yake kukata rufaa Baraza Kuu la Chama kupinga
hatua iliyochukuliwa na Kamati Kuu dhidi yake kumvua nyadhifa zake
ndani ya Chama.
Kuna
sababu mbili za msingi za kukata rufaa;
1.
Utaratibu wa kuchukua hatua za nidhamu ulikiukwa.
2.
Sababu za kuchukuliwa hatua hizo sio sahihi.
Utaratibu
ambao unatakiwa kufuatwa kabla ya kumchukulia hatua za kinidhamu
kiongozi kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Uendeshaji ni kama
ifuatavyo;
Kanuni
ya Uendeshaji 6.5.6 inasema;
Kiongozi
yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka
yake kwa maandishi na mamlaka
husika
na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.
Pia
tunapenda ijulikane kwamba Kanuni ya Uendeshaji 6.5.2 (a), (b), (c)
na (d) kama ilivyorekebiswa Januari 2013 inasema;
Kwa
mujibu wa ibara ya 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba mwanachama yeyote
hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama
kufukuzwa uanachama bila kwanza;
a)
Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika
muda usiopungua wiki mbili.
b)
Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
c)
Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili
baada ya kusikilizwa.
d)
Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia
utaratibu (b), (c) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla
yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwanachama au kiongozi anayelalamikiwa
atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.
Naomba
nichukue fursa hii kufafanua kuwa uongozi wa chama ulifanya mkutano
na waandishi mnamo tarehe 26/11/2013 na kusema kwamba marekebisho
haya ya Kanuni ya mwaka 2013 ambayo nimewawekea hapo juu, ndiyo
utaratibu waliofuata.
Pia
walieleza kuwa sikuwa naifahamu na nilidanganywa kwani Kanuni
ilishabadilishwa.
Mabadiliko
haya ambayo ni katika kipengele (d) kuhusu hatua ya dharura
iliyochukuliwa na Kamati Kuu haikugusa kipengele (a) cha Kanuni.
Yaani ni kuwa hata kama Kamati kuu itachukua hatua ya dharura kwa
mujibu wa kipengele (d), bado kipengele (a) ni lazima ifuatwe na
inatamka wazi sharti la kiongozi kupewa mashtaka kwa maandishi na
kupewa nafasi ya kujibu kwa maandishi. Hii ni haki ya msingi kwa kila
utawala au uongozi.
Mheshimiwa
Zitto Zuberi Kabwe hakupewa mashtaka yake aliyakuta ndani ya kikao
baada ya kupewa taarifa kwa ujumbe wa simu (text message au sms).
Kwa
uzito wa makosa hayo yaliyosababisha kuvuliwa uongozi na kwa
kuangalia athari zake kwake yeye binafsi na chama kwa
ujumla,
Kamati Kuu ilitakiwa kujiridhisha kwamba Kanuni za Uendeshaji na
Katiba zinafuatwa.
Hili
linaendana na utaratibu uliotumika kwa Samson Mwigamba
kuvuliwa
nyadhifa yake ya uenyekiti wa mkoa. Yeye hakuitwa kabisa kwenye kikao
hicho na ni ukiukwaji wa Kanuni ya Uendeshaji
Taarifa
kwa Vyombo vya habari 11/12/2013 Albert Msando 4 6.5.6(d) niliyoisoma
hapo juu kwamba lazima kiongozi huyo aitwe kwenye kikao.
Sababu
zilizotumika ingawaje hajapokea taarifa rasmi ya maandishi kwa mujibu
wa Kanuni za Uendeshaji ni kwamba yeye ameshirki kwenye kuandaa na
kusambaza waraka ambao unasemekana ni mkakati wa ushindi wenye lengo
la kupindua uongozi uliopo.
Waraka
huo haukumtaja Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe kama muandaaji au
msambazaji. Waliouandaa hawajaukana na badala
yake
wamesema waziwazi kabisa kwa maneno na maandishi kwamba Mheshimiwa
Zitto Zuberi Kabwe HAHUSIKI. Sio sawa kumuadhibu Mheshimiwa Zitto
Zuberi Kabwe kwa hisia au tu kwa sababu ya urafiki wake na watu
fulani.
Haya
ni mapungufu ambayo kwa bahati nzuri Katiba na Kanuni za Uendeshaji
zinatoa nafasi ya kurekebishwa kwa kutoa nafasi ya kukata rufaa. Na
utaratibu ni huu hapa;
Kwa
ufupi, Ibara 6.3.6(d) ya Katiba ya Chama; “Kiongozi aliyechukuliwa
hatua za kinidhamu na mamlaka yake ya nidhamu anayo haki ya kukata
rufaa ngazi ya juu ya ile mamlaka yake ya nidhamu na uamuzi wa ngazi
hiyo utakuwa wa mwisho”.
Ibara
6.3.6(e) ya Katiba ya Chama;
“Rufaa
yoyote lazima ifanyike katika muda wa siku thelathini tangu tarehe ya
kupokea rasmi kwa maandishi maamuzi ya mamlaka iliyotoa adhabu”.
Kanuni
za Uendeshaji zinatoa UTARATIBU ambao unatakiwa ufuatwe ili kiongozi
aliyeadhibiwa aweze kutumia HAKI yake ya kukata rufani kwa maneno
haya;
Kanuni
ya 6.5.8 ya Kanuni za Uendeshaji;
“Kiongozi
aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya msingi wa maamuzi ya mamlaka ya
nidhamu ili kumuwezesha kuamua kukata rufani au la”
Kanuni
ya 6.5.9 ya Kanuni za Uendeshaji;
“Mwadhibiwa
atakayeamua kukata rufani atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku
thelathini baada ya kuarifiwa uamuzi wa adhabu”
Kanuni
ya 6.5.10 ya Kanuni za Uendeshaji;
“Baada
ya kutoa uamuzi kikao husika kinalazimika kuandaa
taarifa
kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha ngazi ya
juu.
Taarifa hiyo lazima ifike katika muda wa siku kumi na nne
baada
ya kikao cha mamuzi”
Mpaka
hivi sasa hatujapokea taarifa kamili ya mwenendo wa shauri tokea
kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 20-21/11/2013 Huo ndio utaratibu
ambao Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ameamua kufuata kwa kuheshimu
maamuzi ya Kamati Kuu lakini kukatia rufaa maamuzi hayo. Kuheshimu
maamuzi sio kuyakubali uhalali wake.
Kumekuwa
na matukio ya kusikitisha ambayo mengine yamefikia mahali kuwa fujo
na vurugu ikiwa ni pamoja na kurushiwa mawe Katibu Mkuu wa Chama.
Vurugu hizo baadhi zimehusishwa na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe na
baadhi ya watu.
Mheshimiwa
Zitto Zuberi Kabwe hahusiki kwa njia yoyote na hayo yanayoendelea
na anayakemea na kuwashauri wanachama wote kuwa watulivu na kuendelea
kuwaheshimu viongozi wa kitaifa. Hatua zimeshachukuliwa kukata rufaa
na ni imani yake kwamba Baraza Kuu la Chama litatenda haki kwa
kupitia rufaa yake na kutoa uamuzi.
Nawashukuru
wote.
ALBERT
MSANDO,
Mwanasheria
11/12/2013
0 comments:
Post a Comment