Wakati ulimwengu
ulikuwa ukitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais Mtaafu wa Afrika
Kusini Nelson Mandela mjini Johannesburg kuliibuka kituko ambacho
kilifanywa na Rais wa Marekani pamoja na Mkewe Michelle Obama baada
ya Mke wa Obama kuonesha Wivu wa wazi wazi kwa Mumewe huyo baada ya
kuona yupo busy akipiga Picha na kupiga stori na Waziri Mkuu wa
Danish Helle Thorning-Schmidt .
Kutokana na kitendo
hicho Mke wa Obama alionekana kulitazama Jukwaa huku akiwa hana Time
na kile kilichokuwa kikiendelea lakini kama binadamu alishindwa
kujizuia na kujikuta akihama toka upande wa Kushoto na kwenda kukaa
Upande wa kulia ambapo aliweka uzibe kwa Waziri huyo wa Danish
kuendelea kujiachia na Barack Obama.
Kutokana na mazingira
haya Mitandao mingi ya Ulaya imeandika juu ya kitendo hicho
kilichofanywa na First lady Michelle Obama na kudai kuwa hakikuwa cha
kiungwana.
0 comments:
Post a Comment