Msanii Linah Sanga
ambaye awali alishawahi kuwa katika Mahaba ya Dhati na Msanii
mwenzake wa Bongo Fleva Mwinyi Mkuu amefunguka na kuweka wazi
kuwa
kipindi yupo katika mahusiano na mkali wa Bongo Fleva kutoka THT
Amini hakuwahi kuwaza wala kufikiri kuwa Mzazi Mwenza na mkali huyo
ingawa Amini alikuwa akihitaji Mtoto .
Kwa mujibu wa Linah
amedai kuwa alipokuwa katika uhusiano wa awali hakuwaza kama anaweza
kuwa mama
“Nilipokuwa katika
uhusiano wangu wa kwanza hakuna hata siku moja niliyohisi kama
nitakuja kutamani kupata mtoto maana mwenzangu aliponiambia tuzae
nilimkatalia tofauti na leo hii natamani nishike mimba na ulimwengu
wote ujue kwamba nina mimba,”
Linah Sanga ambaye kwa
sasa walishawekana kando na Amini hajaweza kuweka wazi mahusiano yake
ya sasa ambayo inaonesha kumchanganya kiasi cha kuhitaji kuwa Mzazi
wa huyo mchumba wake wa sasa tofauti na ilivyokuwa kwa Mkali wa
Masauti Mwinyi Mkuu.
0 comments:
Post a Comment