Wednesday, December 11, 2013

SIO MCHEZEA MWILI WA SAJUKI LAKINI ANAFANYA KAZI ALIZOACHA SAJUKI-WASTARA

Msanii wa filamu nchini ambaye mwaka jana alimpoteza mumewe Sajuki baada ya kupatwa Umauti kutokana na ugonjwa ambao ulimsumbua kwa muda mrefu leo
amefunguka katika Page ya EATV katika KIKAANGONI LIVE CHAT na kusema kuwa amekuwa akiona watu wanazungumza mabaya kuwa anatoka Kimapenzi na Bond Bin Suleiman .

Alipoulizwa swali hili na moja ya shabiki kuhusu tetesi hizo mwanadada wastara Sajuki alisema kuwa suala hilo halina ukweli wowote na kudai kuwa Bond ni Meneja wake ambaye kwa sasa anamalizia kufanya kazi alizokuwa ameziacha Mumewe Sajuki kabla ya kufariki dunia.

Si kweli ni meneja lakini sio mchezea mwili wa sajuki lakini anafanya kazi alizoacha sajuki”

Katika moja ya swali aliloulizwa sana Wastara ni kuhusu mahusiano yake ya sasa ambapo watu walikuwa makini kujua kama kuna ukweli wowote juu ya skendo wanazozipata katika mitandao ya jamii na magazeti Pendwa ndipo shabiki mwingine akabandika swali tena Eti kunatetesi kuwa 2mepata shemeji yetu mwingine eti kweli ni mtangazaji wa TV furani hivi ? Na majibu kutoka kwa Wastara yalikuwa kama hivi

Tetesi mtazipata nyingi tu mpka za wazoa makopo sababu sina mume”

Wastara amekanusha skendo kuwa anatoka na Msanii mwenzake wa Filamu ambaye anafahamika kwa jina la Hemed PHD na kusema kuwa Hemed kwake bado ni Mtoto mdogo hivyo atasubili sana pamoja na hao ambao wanahisi anatoka naye.







0 comments:

Post a Comment