Wednesday, December 11, 2013

NIMEKUWA KIMYA ,NIMELALA SANA SASA NIMEAMKA-DAYNA NYANGE

Msaniii katika kiwanda cha Muziki nchini Dayna Nyange ambaye miezi ya karibuni aliingia Bifu na Produza wake Sheddy Clever pamoja na mkali wa Ngololo
Diamond Platnum amefunguka na kusema kuwa amekuwa Kimya sana,amelala sana na sasa anahisi ndio wakati wake kuamka na kufanya yake.

Kauli hiyo ya Mwanadada Dayna Nyange imekuja masaa kadhaa baada ya kutoa Picha ikimuonesha Mwanadada huyo akiwa na Mr Blue akidai kwa sasa wanafanya yao kwakuwa huu ndio wakati wao kufanya yao na watanzania kuelewa niniu wakifanyacho.

Kiukweli nimekuwa kimya sana Nimelala sana ......... Na sasa nimeamka......... ni muda wa kufanya yetu”

aliongeza mkali huyo wa Nivute kwako kuwa kila jambo huwa linakuja na wakati na neema yake hivyo anaamini kuwa huu ndio wakati wake yeye kutamba na kufanya yake pia.

Kila jambo na wakati wake But huu ndo wakati wake "MimiNaWewe" wacha tufanye yetu kwa sababu huu ndo wakati wetu mrbluebyser "MimiNaWewe"

0 comments:

Post a Comment