Wednesday, December 11, 2013

IVO MAPUNDA AWAKANA SIMBA

Kipa namba moja wa Timu ya Kilimanjaro Stars Ivo Mapunda ambaye ni Kipa namba mbili ya Klabu ya Gor Mahia ya Kenya amekanusha kuwa amemalizana na Simba na kueleza kuwa yeye atasaini Mkataba na Timu yake ya Gor Mahia ambayo alikuwa akiitumikia mpaka mkataba wake ulipokwisha siku za karibuni.

Ivo Mapunda alisema tayari viongozi wake wa Gor Mahia wamemfuata na kumueleza wanataka kumpa mkataba mpya wa Mwaka mmoja kuendelea kuichezea Timu yake hiyo.

"Nitabaki Gor Mahia kwa mwaka mwingine mmoja, walinipigia viongozi wangu wakataka kuja kambini nisaini, lakini nikawaambia wasubiri nimalize mashindano ya Kombe la Chalenji,"

Hata hivyo, kipa huyo ambaye mashabiki wa Gor Mahia wamekuwa wakiushinikiza uongozi wa timu hiyo kumsajili, hakuwa tayari kutaja dau ambalo atapatiwa na klabu yake hiyo.

0 comments:

Post a Comment