Wednesday, December 18, 2013

YANGA KUMKOSA OKWI NANI MTANI JEMBE

Mwenyekiti  wa Kamati nya Mashindano na Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb amesema si lazima mshambuliaji wao mpya Mganda Emmanuel Okwi acheze
mechi ya 'Nani Mtani Jembe' dhidi ya watani wao wa jadi, Simba itakayochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Bin Kleb alisema kuwa baada ya kukamilisha usajili wake Yanga, Okwi aliwaomba amalizie shughuli zake kwanza kabla ya kutua nchini kuwatumikia mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

"Ninashangazwa na taarifa zinazoenezwa kwamba Okwi anatua nchini leo (jana) mchana kwa sababu bado anamalizia shughuli zake nchini kwao (Uganda).


"Kama akiwahi na kocha akaamua kumpanga katika mchezo wa Jumamosi, haina shida, atacheza mechi hiyo. Ila Leo) ndiyo atatueleza siku yake ya kuja Tanzania," alifafanua zaidi kiongozi huyo ambaye amefanikisha usajili wa wachezaji muhimu katika kikosi cha kocha Ernie Brandts akiwamo 'kiraka' Mbuyu Twite.

0 comments:

Post a Comment