Baada ya kuwa kimya
muda mrefu kwa kuondokewa na mumewe (Sajuki) , Wastara leo kupitia
Mitandao ya Kijamii amefunguka ya
moyoni kuwaomba watanzania
wamuombee aliyekuwa mumewe Marehemu Sajuki aliyefariki mwaka jana
Tarehe 2 January.
“Siku week mwezi hatimae mwaka unaingia
tokea ukimbie mikononi mwangu mwetu, milele nitakukmbuka daima nahisi
uko sehemu nzuri unanisubiri, tal 2/1/2014 my bld anatimiza mwaka
tokea atutoke katika hii dunia, nawaomba tuwe pamoja katika duwa
itakayofanyika mkoani songea kokote ulipo inua mikono kumuombea juma
kilowoko aka sajuki and mboni ya wastara”
Ni wazi kuwa Wawili
hawa walipendana kwa dhati huku kila mmoja akiwa na imani na mwenzake
kwa asilimia zote ndio maana miaka itapita lakini kumbukumbu ya Juma
Kilowoki haiwezi kufutika kwa wepesi kwa Wastara kutokana na ukweli
kwamba Sajuki alikuwa na mapenzi ya dhati kwa mkewe huyo ambayo kwa
namna moja au nyingine wamepitia naye magumu mengi ambayo yapo
tuliyoyashuhudia.







0 comments:
Post a Comment