Mwenyekiti wa Young
Africans Yusuf Manji leo amemtambulisha rasmi Bw. Beno Njovu kuwa
katibu mkuu mpya wa klabu akichukua nafasi ya Lawrence
Mwalusako
aliyekua kaimu katibu mkuu kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Akiongea na waandishi
wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, Mwenyekiti wa Yanga Bw.Yusuf
Manji amesema Beno Njovu anaanza kuitumikia hiyo nafasi mpya kuanzia
leo na Mwalusako atakua nae pamoja kwa kipindi cha mwezi mmoja mpaka
atakapokabidhi kazi rasmi.
Aidha Manji ametangaza
mkutano mkuu wa wanachama Januari 19,2013 ambapo wanachama watapata
fursa ya kupitia mapato na matumizi, na ajenda zingine mbalimbali
ambazo zitajadiliwa katika mkutano huo.
Kikao cha kamati ya
utendaji kilichoketi mwishoni mwa wiki kimemteua Bw.Seif Ahmed
"Magari" kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya
Kimataifa na kutokana na nafasi hiyo pia ameteuliwa kuwa mjumbe wa
Kamati Kuu ya Utendaji wa klabu ya Yanga.







0 comments:
Post a Comment