Msanii
Rama Dee ambaye kwa sasa anaishi Nchini Australia amefunguka na
kusema kuwa Majukumu ya shule ndio sababu ya yeye kuchelewa kufanya
Video
ya Wimbo wake Kama Huwezi ambao umefanya vizuri katika Radio
Station mbalimbali Tanzania.
“Nimechelewa
kufanya Video ya Kama huwezi kutokana Na majukumu ya kimasomo naomba
tuwe Na subira Ndugu zangu hiyo ndio sababu ya msingi”
Kama
huwezi ni Wimbo uliotoka Katikati ya mwaka huku akiwa amempa shavu
Mwanadada LadyJaydee na kuweza kupenya katika kila kona kutokana na
umahiri wa wakali hao wawili walioshirikiana vizuri kutengeneza kitu
kizuri na kuwakonga nyonyo Watanzania.
Lakini
licha ya Kusongwa na masuala ya shule Rama Dee ameeleza kuwa hivi
karibuni ataanza tena kufanya kazi za sanaa kwa kuwa atapata muda wa
kufanya hivyo.
“Ratiba
yangu ya kufanya mziki itaanza tena karibuni...Mipango ya kuifanya
video ya Kama Huwezi niliisimamisha kutokana na majukumu ya shule”








0 comments:
Post a Comment