Kiungo
Mshambuliaji wa Yanga Haruna Niyonzima 'Fabregas' amefunguka na
kusifu uongozi wa Yanga Kumuongeza Mchezaji Emmanuel Okwi katika
kikosi cha
'Wanajangwani',Mshambuliaji huyo amekili na kufurahi
kuongezewa nguvu ya wachezaji matata ambao kwa pamoja wanaunda Kikosi
cha Jangwani.
"Siamini
kama kweli Okwi ametua Yanga, ni usajili makini kwa ajili ya
mafanikio ya timu hasa katika mashindano ya kimataifa. Yanga itatisha
kwa sababu sasa imekamilika kila idara," alisema Niyonzima
ambaye jana ndiyo ilikuwa siku yake ya kwanza kujifua na kikosi cha
kocha Mholanzi Ernie Brandts tangu arejee akitokea kwenye mashindano
ya Kombe la Chalenji.






0 comments:
Post a Comment