Tuesday, December 17, 2013

MAAMUZI YA AFANDE SELE KUMUACHA MKEWE NAKUJIFANANISHA NA NELSON MANDELA WANANCHII WAMEMCHANA.

Siku za hivi karibuni Msanii Afande Selle aliweka wazi kuwa ameachana na Mkewe ambaye ameishi naye kwa miaka 15 na kubahatika kupata watoto
wawili,katika tetesi zilizopo zinadai kuwa Baba Tunda ameshindwa kuendelea kuishi na Mama Tunda kutokana na mabadiliko ya Tabia ya Mama Tunda ambaye ndiye aliyekuwa Mke wa Afande Selle.

Afande Selle ambaye kwa sasa ameanza kujikita katika Siasa amejifananisha na Hayati Nelson Mandela kwa kumpiga chini Mkewe huyo na kuingia rasmi katika Siasa lakini wadau mbalimbali wamedai kuwa maamuzi aliyofanya Afande Selle yamesukumwa na Bangi tu na si akili yake ya kawaida.

Bin Diesel Aende kwanza jela miaka 27 akirudi ndio amuache mkewe hapo ndio aanze kufikiria kufanana na mandela .Nguvu ya bangi hyo Mandela alikuwa mtu mkubwa dizaini ya kina Mwl.nyerere Leo mvuta bangi tu anajifananisha nae kisa kaachana na mkewe tena anapaswa kushtakiwa.


Wema Christian Szczesny Mibange yao tu hiyo na mwenzie 20%

Peter Charles Millanzi hahahaha amejifananishaje na mandela kwani huyo mkewe alimsaliti kama ajamsaliti mwambieni aache ujinga alee familia yake wasije wakawa omba omba bure .


John Francis Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "tatizo lenu mnaacha mambo mazuri tuliofanya mnaiga mambo mabaya tuliofanya"

Edfredson Nkwama Manchester bangi zinamsumbua mwambie asije akawa chz tu.

Beny Mfinanga Usifanye ivyo kk kwan ktk maisha kuwalea watt inahitajika malez ya wazaz wote wawl. Ili kufankisha malengo ya mtoto, kama mama tunda kakukosea inapaswa msamee maisha yaendelee kk nihayo tu.

0 comments:

Post a Comment