Thursday, December 12, 2013

NYOTA YAKO LEO IJUMAA : 13/12/2013

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Utakuwa katika wakati mgumu mno wa kuamua jambo ambalo umeshawishiwa na mpenzi wako au rafiki yako wa karibu, hadhari na uamuzi utakaouchukua
unaweza kupata balaa. Lazima katika mambo yako uwashirikishe wazee ndio utafanikiwa.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Wachunge sana watoto wako kwani kuna uwezekano wa watu kuwafanyia kitu kibaya au kuwashawishi kufanya vitu vibaya.Hakikisha unawachunga watoto usiwape nafasi ya kuwa peke yao wanaweza kudanganywa.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Ikitokea leo wakati wowote ukaona kitu cha kukufurahisha, au kitu ambacho kitakufanya ucheke, hiyo itakuwa ni dalili ya kupata safari ya mbali ambayo umekuwa ukiisubiri kwa muda mrefu

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Leo utatukuzwa kwa jambo ambalo hukulifanya.Wewe kaa kimya na kubali kutukuzwa huko wala usikatae. Kuna kila dalili ya kupata mafanikio katika malengo yako uliyoyapanga kwa wiki nzima.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Pendelea kujipa upendeleo fulani katika shughuli zako za kila siku, kuna dalili ya kupata cheo. Jaribu kushirikiana sana na wanawake kuna mambo mazuri utayapata kutoka kwao hasa katika siku ya leo.

NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Leo ukipata salamu zozote kutoka kwa mmoja katika ndugu wa familia yako, hiyo ni dalili ya kupata kitu kizuri na biashara zako kukuendea vizuri, Jaribu kuwa mkarimu kwa kila atakaekujia na kukueleza shida yake.

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Siku ya leo unatakiwa kufanya mambo mapya ili kujipatia kipato, mambo yako ya zamani ni bora ukayaacha kwanza au kuyapanga upya kwani hayafai na wala hayakusidii. Jaribu kuwatembelea wazee wako upate baraka zao kwa kila jambo unalotaka kulifanya

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Mipango yako itaendea kama ulivyopanga bila ya kuingiliwa na mtu au vikwazo vyovyote, Sharti ni moja tu fanya mipango hiyo iwe ya siri usimhusishe mtu. Uhusiano ambao umevurugika kati yako na Mpenzi wakosa utatengemaa.

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Kuna kila dalili ya kupata kila kitu ulichokuwa anakitaka kutoka kwa mpenzi wako, Jaribu kuwa nae karibu na mbembeleze aweze kukufanyia mambo mazuri ya kimaisha.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Leo kuna ugomvi wa kimapenzi. Unashuriwa kuwa makini kwa vile sasa mapenzi yako yatakuwa ya kugombana gombana, unashauriwa kuwa mtulivu na jiepushe na kujibishana kila wakati hasa na mkeo, mumeo au mpenzi wako.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Jaribu kupata ushauri wa kisheria kwa kila jambo unalotaka kulifanya.Mipango yako yote lazima ipitie kwa Wakili au Hakimu vinginevyo utadanganywa au kutapeliwa. Mambo ya mirathi ipe kipaumbele usiidharau utanufaika.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Unahadharishwa uwe mwangalifu na mkeo au mumeo na rafiki yako kwani wanampango wa kukugeuka na kukuhujumu, fanya mambo yako bila ya kuwashirikisha kwa kipindi hiki. Weka utaratibu wa kurudi nyumbani mapema.

0 comments:

Post a Comment