Thursday, December 12, 2013

BEYONCE AWASHANGAZA MASHABIKI ULIMWENGUNI KWA KUTOA ALBUM KIMYA KIMYAAA.

Mwanamuziki Beyonce ambaye ni mke wa Mwanamuziki Jay Z amewashangaza Mashabiki wake duniani baada ya kuachia Album yake inayokwenda kwa jina la
BEYONCE Kimya kimya bila kutoa taarifa yoyote ile juu ya kuachia kwa Album hiyo.
 
Utamaduni uliozoeleka duniani kwa Mwanamuziki mkubwa huwa wanatoa taarifa juu ya maandalizi ya Album au Single Fulani lakini kwa mwanadada Beyonce imekuwa tofauti kidogo kwani hakutoa taarifa youyote ile juu ya kuachia kwa Album hiyo bali ameiachia Kimya kimya .

Katika Album hiyo yenye Nyimbo 14 ambayo amewapa shavu wasanii wengine wakubwa kama Jay Z,Drake,Frank Ocean,Timbaland, Michelle Williams, Kelly Rowland, Justin Timberlake,na wengine kibaooo.

Nyimbo zinazopatikana katika Album hiyo mpya ya Beyonce ni kama zifuatavyo
1) Pretty Hurts
2) Haunted
3) Drunk in Love (feat. Jay Z)
4) Blow
5) No Angel
6) Partition
7) Jealous
8) Rocket
9) Mine (feat. Drake)
10) XO
11) ***Flawless (feat. Chimamanda Ngozi Adiche)
12) Superpower (feat. Frank Ocean)
13) Heaven
14) Blue (feat. Blue Ivy)

0 comments:

Post a Comment