Friday, December 13, 2013

BAADA YA KUANDAMWA SANA ZITTO KABWE LEO AMEANDIKA HIKII.

Baada ya kuandamwa na mambo mbalimbali katika Chama cha Demokrasia na Maendelea Mbunge wa Kigoma Kaskazini Leo ameandika Quatation ambayo kwa
namna moja au nyingine inatoa Picha ya wazi kuwa katika Mvutano na magumu anayopitia sasa kama Mwanachama wa Chadema na Baadhi ya Viongozi wa Chama hata baadhi ya wafuasi wa chama hicho kuwa ni mapito tu na atashinda mwisho wa siku.
 
"First they ignore you, then they laugh at you, then they fight you, then you win".
Mahatma Gandhi .

Kwanza watakukataa,watakucheka,baadaye watapigana na wewe au kugombana na wewe lakini mwisho wa siku Utashinda.

Hivi karibuni Kamati kuu ya Chadema ilimvua nyazifa Zote Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe na kumuandikia Barua ya kujieleza ndani ya siku 14 kwanini alisivuliwe wanachama wa Chadema.

Lakini pia Mbunge huyo wa Kigoma alishawahi kutoa taarifa kuwa anawafahamu kwa majina watu ambao walificha Mamilioni ya Pesa Nje ya Tanzania lakini lakini sakata hili nalo limechukua sura mpya baada ya Viongozi mbalimbali wakidai kuwa Mh Zitto hana taarifa za watu hao na kumtaka apewe adhabu kwa kulidanganya Bunge kuwa anamajina ya watu walihusika kuficha pesa za Umma nchini Uswizi.

0 comments:

Post a Comment