Thursday, December 12, 2013

IVO MAPUNDA MCHEZAJI MPYA SIMBA

Klabu ya Simba Jana ulifanikiwa kuwasajili wachezaji wawili kutoka Klabu ya Gormahia ya Nchini Kenya,Wachezaji hao ni Kipa Ivo Mapunda na beki wa kati
wa Gormahia,Donald Mosothi.

Baada ya Klabu ya Gormahia kudai kuhitaji kumuongezea Mkataba Kipa Ivo Mapunda na kufanya nao mawasiliano ya kutaka kusaini mkataba tena katika Klabu hiyo ya Gormahia Uongozi wa Simba ulilazimika kumlipa Pesa Mke wa Ivo Mapunda kiasi cha Million 15 ili kumuhakikishia kuwa wanamuhitaji ajiunge na Simba na baadaye uongozi ulifunga safari mpaka Kenya kwenda kumsainisha mkataba huo.

"Tayari tulishamkabidhi mke wake shilingi milioni 15,000 jijini Dar es Salaam jana (Jumatano) kabla ya kuja huku (Nairobi)," Katibu Mkuu wa Simba Mtawala alisema.

Katibu Mkuu huyo alisema wamelazimika kuja jijini hapa kumsajili baada ya kusikia kuwa klabu yake ya Gor Mahia ina mpango wa kumwongeza mkataba mpya.

0 comments:

Post a Comment