Yanga
SC imempata mshambuliaji huyo msumbufu kwa mabeki wengi kwa mkataba
wa miaka miwili na nusu ambapo kwa sasa ataitumika klabu yake mpya ya
watoto wa jangwani mpaka mwishoni mwa msimu wa 2015/2016.
Dirisha
dogo la usajili nchini Tanzania limefungwa leo usiku wa Disemba 15,
2013 saa 6 usiku ambapo mabingwa wa kihistoria klabu ya Yanga
wamekalilisha taratibu zote za usajili ikiwa ni pamoja na kupata hati
ya uhamisho wa kimataifa maarufu kama ITC.
Usajili
wa Emmanuel Okwi unaifanya timu ya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji
watano wa kimataifa wakiwemo mganda mwenzake Hamis Kiiza, Haruna
Niyonzima, Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu.
Uongozi
wa Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki kuwapa ushirikiano
wachezaji wote wa zamani na wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo
la usajili.
0 comments:
Post a Comment