Friday, December 13, 2013

FID Q AWACHANA WANASIASA SOMA ALICHOKISEMA HAPA

Mwanamuziki Fid Q ambaye anawakilisha Mwanza katika Muziki wa HiP Hop na kuibeba Tanzania katika Hip Hop amefunguka na kuweka wazi kuwa wanasiasa
wa Tanzania wengi wameweka Masirahi yao mbele kuliko hata maslahi ya Taifa au watu wanaowatumikia.
 
Mwanamuziki huyo ameonesha Kuwapuuza wanasiasa kwakuwa wanachokitenda ni tofauti na imani yake na kile ambacho yeye anakiamini ila ili kwenda nao sawa na kutokuvunja heshima yao muda mwingine anajifanya kama hawaoni wanavyofanya michongo yao ya kupiga pesa za Umma.

Wanasiasa wabongo washanidissapoint siku nyiiiiingi sana..Na ili nisionekane HATER.. Nimeamua kujifanya siwaoni wanavyojipigia 'mahela' yao”
 
akiwa anajaribu kufafanua kwa makini suala hili FID Q alisema kuwa Ni ukweli Hawa wanasiasa wa Tanzania Wana imani yao ile ya ' aaah huyo mwenyewe angepata hii nafasi angejipa shavu '.

Hivyo kutokana na Imani hiyo ndiyo inayowapelekea Kuifisadi Nchi na kupiga Dili ambazo wanaingiza Pesa kuliko hata kutatua Matatizo ya Wananchi waliowapa Nafasi huku wakitegemea wanasiasa hao kuwa Mabolozi9 wazuri kuwawakilisha na kutatua matatizo yanayowakumbuka katika Jamiii.


Napiga nao story tu kwasababu nao ni watu-> UbinadamuKazi

0 comments:

Post a Comment