Wednesday, November 13, 2013

WATAKE WASITAKE KASEJA NI KIPA BORA TANZANIA-PONDAMALI.

Kwa mujibu wa Kocha wa Taifa Stars Juma Pondamali amefunguka na kusema kuwa amependezewa sana na kitendo cha Timu ya Yanga kumsajili aliyekuwa
Kipa Namba moja wa Simba Juma Kaseja ambaye kwa msimu uliopita wa Ligi hakuweza kuichezea Simba kutokana na kumaliza mkataba nao na kutomsainisha tena.

Juma Kaseja wiki iliyopita alisaini mkataba wa miaka miwili na Klabu ya Yanga ambayo awali alishawahi kuichezea kwa Msimu mmoja kati ya Mwaka 2008/9.
Kwa mujibu wa Pondamali alisema Kaseja ni mchezaji anayejituma na anayefanya mazoezi kwa muda wa saa sita kwa siku hivyo watake wasitake hakuna Kipa anayeweza kuwa kama Kaseja kwa sasa.

"Ni mchezaji wa pekee, na kwangu ndiye kipa bora hapa nchini, watake wasitake,"



0 comments:

Post a Comment