Mbunge
wa Kawe Halima Mdee amefunguka leo na kusema kuwa wasanii wa Bongo
wasipokuwa na umoja katika Kazi zao za Sanaa kila siku
wataendelea
kuumizwa na wajanja wachache wanaotumia sanaa kujinufaisha wenyewe
kauli hiyo imetolewa na Mbunge huyo kufuatia Wasanii hao kutotilia
umuhimu mambo ya msingi ambayo yanahusu sanaa zako.
Kwa
mujibu wa Mdee kuna wasaniii walialikwa kwenda kushiriki kuchangia
Maoni yao juu ya Sheria ya sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza
(1976) lakini katika Wasanii ambao walipewa mualiko huo hakuna hata
mmoja ambaye alifika kuchangia katika Ngazi ya kamati ambapo walikuwa
na nafasi ya kuchangia.
“Tulialika
wasanii katika ngazi ya kamati waje kutoa maoni ...hawakujitokeza .
Leo
wakati Wabunge wakijadili Mabadiliko ya Sheria ya Filamu na Michezo
Msanii mmoja wa Filamu ambaye anafahamika kwa jina la Batuli alihoji
kwanini baadhi ya wasanii hawajaonekana Bungeni ndipo alipojibiwa
kuwa hata vikao vya msingi ambavyovingewapa nafasi ya kuchangia
hawakuweza kutokea.
Mbunge
Halima Mdee aliendelea kusema kuwa wasanii wanapaswa kuifanyia kazi
changamoto waliyonayo ya Kugawanyika na wanapaswa kuwa kitu kimoja
ili waweze fanikisha Mambo yao na kujikomboa katika matatizo lukuki
yaliyowazunguka.
“Ni
changamoto ambayo inabidi muifanyie kazi. Bila umoja,mtaendelea
kuumizwa!”







0 comments:
Post a Comment