Taarifa
zilizotufikia kutoka katika vyanzo mbalimbali zimesema kuwa, wananchi
wa kata ya Ubaruku wilayani Mbarali Mkoani Mbeya wamezusha mapigano
ya
wenyewe kwa wenyewe kutokana na kitendo cha Walinzi wa Shamba
NAFCO Mbarali kumuuwa kwa kumpiga Risasi Mtu Mmoja kwa kupita sehemu
iliyozuiliwa.
Kutokana
na Mapigano hayo yaliyoanza jana kufikia Leo Asubuhi zaidi ya Nyumba
Tatu ziliteketezwa kwa moto na Wananchi wenye Hasira .
HAYA
NI MAONI MBALIMBALI YA WANANCHI WA MBARALI JUU YA MUWEKEZAJI HUYO
KATIKA SHAMBA LA NAFCO MBARALI.
SIMANZI
KUBWA..."Katika hali isiyokuwa ya kawaida kumekuwa na
sintofahamu ndani ya wilaya yangu ya Mbarali (Mbeya) sehemu
nilipozaliwa UBARUKU ( nyumbani ) tangu eneo la shamba la mpunga
ambalo lilikuwa likimilikiwa na serikali kubinafsishwa kwa mtu mmoja
ambaye naweza sema ameshindwa kuliendesha shamba hilo.
Hii
inatokana na migogoro ambayo imekua ikijitokeza mara kwa mara tangu
kuingia kwake na baadhi ya watu wamepoteza maisha na wengine wengi
kujeruhiwa.... ni mambo mengi sana hapo katikati yamejitokeza,
wanasiasa wamefanya ya kwao lakini mwisho wa Siku Wanambarali,
wananchi wa kawaida ndio tunao athirika...
kubwa
zaidi ni hili ambalo limejitokeza sasa; Kwa taarifa nilizo nazon ni
kwamba Jana mtu mmoja ameuawa katika eneo hilo la mwekezaji tena
inavyosemekana ni kwa kupigwa Risasi na walinzi wa mwekezaji huyo,
binafsi naumia sana hasa pale ambapo naona Shamba ambalo limebeba
historia kubwa sana ya maisha yangu, shamba ambalo limenifanya leo
hii kufikia hapa nilipo, leo hii limegeuka kuua watu wasio na hatia
eti kisa amekabidhiwa mtu mmoja asiyejali utu wa wanambarali,
inaniuma sana...
Nawapa
pole sana wafiwa na wahanga wa vurugu zilizojitokeza na wana mbarali
wenzangu kwa ujumla ambao kwa namna moja ama nyingine wameathirika
kwa vurugu hizo, Nawaomba ndugu zangu wa Mbarali kuwa na Umoja,
Hekima na Ushirikiano katika harakati za ukombozi wa Mbarali yetu,
pia nawaombea na kuiombea Mbarali irudie enzi zake za Amani na Upendo
kwa kila mtu.....Mungu ibariki Mbarali, Mungu ibariki Tanzania...








0 comments:
Post a Comment