Wednesday, November 27, 2013

TFF KUMUWEKEA NGUMU JUMA KASEJA AU DILUNGA KUSAJILIWA YANGA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Limeonesha nia ya kutaka kuweka ugumu kwa Klabu ya Yanga baada ya kuwasajili Wachezaji wake Wawili Juma Kaseja na Dilunga.
Shirikisho la Mpira wa Miguu kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura limetoa taarifa kuwa kitendo cha Vilabu kupeleka wacheazaji wake katika Vilabu vingine haitoi nafasi ya usajili kwa Mchezaji mwingine.

"Kama klabu ilisajili wachezaji 30 maana yake ni kuwa, haina nafasi ya kuongeza wachezaji. Kwa upande wa wachezaji wa kigeni (foreign players), tunakumbusha kuwa, kuanzia msimu ujao 2014/2015 watakuwa watatu tu badala ya watano wa sasa,"


Tamko hilo la TFF lina maana kwamba, Yanga kwa sasa tayari imeingia mikataba ya kuwasajili kipa Juma Kaseja aliyekuwa huru na kiungo Hassan Dilunga kutoka Ruvu Shooting, haitakubaliwa kumsajili mmoja wa wachezaji hao kwani tayari ilikuwa na wachezaji 29.

0 comments:

Post a Comment