Tuesday, November 26, 2013

TANESCO YAKANUSHA KUPANDISHA BEI YA UMEME

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limekanusha Vikali Taarifa iliyosambazwa katika vyombo mbalimbali vya Habari kuwa Serikali imepandisha Bei ya Umeme
hadi kufikia Shiling 800 kwa Unit Moja.



Ukweli ni kwamba TANESCO bado haijapandisha bei ya umeme ila imepeleka maombi ya kuomba kuongeza bei ya umeme kwa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) na si serikali.”

Hatua hii imefuatiwa baada ya Shirika la Umeme Kuanza kupata taarifa kutoka kw wadau mbalimbali na wateja wao walipokuwa wakihoji na kujiuliuza kwanini Bei ya Huduma ya Umeme imepanda mara dufu pasipo kufuatwa kwa utaratibu na kanuni za Kupandisha Umeme.



0 comments:

Post a Comment