Klabu
ya Simba ambayo alipigwa faini ya kulipa gharama ya Sh Million 25
kutokana na uhalibifu wa Uwanja uliosababishwa na Mashabiki wa Simba
katika
Mechi waliyocheza na Kagera Sugar Oktoba 31, mwaka huu na
kutoka kwa sare ya 1-1.
Msemaji
wa Simba alifunguka na kusema kuwa wameomba muda wa kufanya malipo
hayo uongezwe ili wapate kufanya tasmini kama ni kweli uharibufu huo
unaendana na gharama wanazotakiwa kulipa.
Mbali
na hilo msemaji huyo alifunguka na kusema kuwa Kikosi cha Polisi
Kilichokuwepo Uwanjani hapo siku ya Tukio nacho kilikuwa chanzo kwa
kuongeza uharibifu huo kwani walipaswa kutumia njia nyingine kutuliza
vurugu zilizokuwepo kwa mashabiki uwanjani hapo na si kutumia Mabomu
ya Machozi ambayo ndiyo yalifanya vurugu kuongezeka maradufu.
Kwa
nini askari walipiga mabomu katika jukwaa hilo na kusababisha watu
wakimbie ovyo huku wakikanyaga na kuharibu viti uwanjani? Je,
hapakuwa na namna nyingine ya kudhibiti vurugu hizo badala ya kutumia
mabomu ya machozi?" Alihoji Kamwaga.







0 comments:
Post a Comment