Timu ya Mbeya City
ambayo katika Msimamo wa Ligi Kuu Vodacom Bara ipo nafasi ya Pili
huku ikiibuliza Simba na Yanga na katika msimamo wa Ligi.
Mbeya City leo
anakutana na Mwenyeji wake Azam FC katika uwanja wa Chamanzi Jijini
Dar es Salaam katika Mechi zinazoendelea za Ligi KUU Vodacom,Uongozi
wa Mbeya City amesafiri na mashabiki zaidi ya 300 wakitokea Mbeya
kuja kutoa Support kwa Timu yao ambayo ndiyo imepanda daraja na
kushiriki Ligi kuu Tanzania Bara Mwaka huu.
“Tumejipanga na
tunauchukulia mchezo huo kwa umuhimu mkubwa kwani tumeona jijini
Mbeya timu inasapoti kubwa kutoka kwa mashabiki, kwa nini ugenini
tusiisapoti ndio tukajipanga na kuamua kuja Dar es Salaam ili
kuhakikisha Azam anakufa Alhamisi kwa mabao 2- 0,” alisema.
“Tumekodi
mabasi 10 kwa ajili ya mashabiki ili kuisapoti timu, tumefunga
safari ya saa 12 kutoka Mbeya kuja Dar kuishangilia timu,”
alisema Mastala huku kocha wa timu hiyo, Juma Mwambusi akiahidi
kupambana kiume uwanjani.







0 comments:
Post a Comment