NGE - SCORPIO
(OCT 24- NOV 22)
Leo ni siku nzuri kwako Mpenzi wako atarejea
salama, na utashinda mitihani na adui yako atajuta Hii ni wiki nzuri
ya kurekebisha makosa yote ambayo umeyafanya katika kipindi cha
nyuma.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Siku ya leo
Unashauriwa kuwa kufanikiwa kwa mambo yako kunahitaji wewe uanze
kujishughulisha na mambo hayo mara moja wala usisite site.Jambo baya
kwako ni kuwa kama kuna mgonjwa hapo nyumbani kwako, lakini kama kuna
mjamzito basi atazaliwa mtoto wa kike
MBUZI - CAPRICORN (DES
22 – JAN 20)
Mambo yote unayoyataka yatatimia kati ya leo na
Jumanne au Jumamosi ijayo usiku. Pengine katika mwezi wa novemba
Tegemea kujionea mambo mengi ambayo ulikuwa umefichwa kwa muda mrefu
na watu wako wa karibu. Ili kuleta baraka leo nenda kawatembelee
wazee wako.
NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Leo
utapata fedha au utapata faida ambayo hukuitegemea au utasamehewa
madhambi uliyomfanyia rafiki yako. Furaha yako uliyonayo ni ishara ya
mambo yako kwenda vizuri kama ambavyo umekuwa ukitarajia
SAMAKI
– PISCES (FEB 20- MACH 20)
Siku ya leo unawaza juu ya nafsi
yako,unataka kujua maisha na hali yako itakuwaje. Pana kazi au jambo
ambalo unashaka nalo kama litatimia au vipi? Elewa kwamba utapata
mkosi kazini kwako au utaletewa biashara ambayo itakuletea balaa
kimaisha Siku hii ya leo kuna mgeni na kitu kilichopotea ambacho
unataka sana kujua habari zake.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR
20)
Wiki hii una hamu sana ya kukutana na mpenzi wako na kujua juu
ya safari au biashara na kazi. mambo yako yataenda kombo, Unashauriwa
kuwa mtulivu na hali hiyo kwa kuwa ni hali ya muda mfupi tu.
NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Leo Haja yako
itatimia. Kuna mtu mkubwa wa hapo ndiye atakaye kuonea huruma kwa
njia usiyoitegemea. mgonjwa wako aliye hospitali atazidiwa au
utaletewa habari ya mbaya za kifo cha mgonjwa.
MAPACHA -
GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Siku ya Leo Mambo yote unayotaka
utayapata kwa sharti uache kuwa na wasiwasi na hofu au kupapatika,
mambo yako mengi yatakwenda kwa kusuasua, Unashauriwa kuwa makini na
kila unachotaka kukifanya, usimamizi wa karibu unahitajika kwa kila
jambo unalotaka kulifanya.
KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Siku
ya leo lazima utapata kitu unachokitaka au pesa unazohitaji au mtu
unayemtarajia. Mtoto au kitu kilichopotea kitarejea mambo yako mengi
yatasimama, yale tu utakayoyafanya wewe mwenyewe ndiyo
yatakayofanikiwa, lakini yale yote utakayoyaagiza yafanywe na watu
wengine yatalala.
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Siku ya
leo Lazima utapata kitu unachokitaka au pesa unazohitaji au mtu
unayemtarajia. Mtoto au kitu kilichopotea kitarejea lakini tahadhari
utapatwa na balaa la kupigwa bila ya kutegemea na bila kosa lolote na
hata kama lipo kosa basi kosa hilo hukulifanya wewe.
MASHUKE -
VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Siku ya leo,itakubidi utoe rai nzuri na
uache woga na usivunjike moyo kwani patatokea upinzani na undani,
kuna habari za uongo utaambiwa na Mkeo au Mpenzi wako kuhusiana na
biashara zako. Jaribu kufanya uchunguzi kabla hujachukua
hatua.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo ni siku
unayopaswa kuwa makini zaidi na na kazi zako, kuna uwezekano wa
kuingia kwa hasara Safari unayofikiria ni nzuri, biashara yako
itafanikiwa lakini maendeleo yako yatakuwa ni madogo na yatakuwa
yanaenda polepole sana.
(Imeandaliwa na
Mtabiri Maalim Hasan)
0 comments:
Post a Comment