Sunday, November 3, 2013

SERIKALI IMESEMA DIVISION O IKO PALE PALE NA HAKUNA DIVISON V KULIKUWA NA MAKOSA KATIKA KUTANGAZA

Wakati wanafunzi wa Kidato cha Nne wakiwa wanaendelea na  kufanya mitihani yao ya mwisho Nchi nzima huku wakiwa na imani kwa kuanza kutumia
madaraja mapya ya ufauru baada ya Wizara ya Elimu kutangaza madaraja hayo mapya ambayo yalikuwa hayana Division 0 lakini leo Bungeni Naibu waziri wa Elimu Philip Mulugo amekanusha taarifa zilizotolewa na Katibu mkuu Wizara ya Elimu na kusema kuwa hakuna Division V na Divison 0 iko palepale.
Naibu waziri amesema kuwa ulitokea mkanganyiko katika kutoka taarifa hizo.


Awali, Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) lilikuwa likitumia alama A, B, C, D na F huku alama A ikianza na maksi wa asilimia 81-100, B=61-80, C=41-60, D=21-40 na F=0-20. Aidha kulikuwapo na madaraja ya I, II, III, IV na 0.

Kwa mujibu ya mabadiliko hayo yaliyotangazwa wiki iliyopita na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, alama zitashuka ambapo alama A itakuwa ni (75-100),B+ (60-74), B (50-59),C (40-49), D (30-39), E (20-29) na F (0-19).

0 comments:

Post a Comment