Ingawa
kuna taarifa kuwa Mzunguko wa Pili wa Ligi kuu Vodacom Bara Timu ya
Simba inaweza kunolewa na Kocha Patrick Phiri lakini mwenyekiti wa
Simba
Ismail Aden Rage amefunguka na kusema kuwa kweli kutakuwa na
mabadiliko lakini kidogo.
"Tutafanya
mabadiliko kidogo, lakini Kibadeni ataendelea kuwa kocha mkuu wa
Simba.
Tumekuwa na utaratibu wa kuvunja mikataba ya makocha wetu
katikati ya misimu hali ambayo imekuwa ikisababisha kuyumba kwa timu
yetu. Hatuko tayari kuona makosa hayo yakijirudia,"
Timu
ya Simba Imeweza kumaliza Msimu wa kwanza wa Ligi huku ikiwa
imeshikilia Nafasi ya Nne Katika Ligi Nyuma ya Yanga,Azam na Mbeya
City lakini mpaka msimu wa Kwanza wa Ligi unakwisha Kocha Kibadeni
King hakuweza kupata Fisrt Eleven.







0 comments:
Post a Comment