NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Ili matatizo yako yafanikiwe. Kwanza itakubidi umpate mtetezi au wakili na usione
haya kutaka msamaha na kumsifu anae husika Karibisha
wageni, fanya vitendo vizuri saidia sana haja za watu.Ili matatizo yako yafanikiwe. Kwanza itakubidi umpate mtetezi au wakili na usione
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 21)
Hivi karibuni kuna mtu unaetaka kukutana nae lazima mtakutana lakini itakubidi umfuate, akija mwenyewe basi mwinukie atakuwa anatoka upande wa Magharibi au Kusini na atakuja sasa au jioni, anaweza kuwa mpenzi au mtu mtakaesikilizana sana.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Kama unamipango na mtu yoyote usione shaka kumkabili au kumtolea shida zako utapata haja yako mara moja kama si leo, Jumatatu au Mwezi wa Juni lakini itatimia.Elewa kuwa pana mtu anaitwa Yusufu au Joseph atakusaidia na lazima ushirikiane nae.
NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Kama kuna mtu unayetaka kushirikiana nae jina lake linaanza na moja ya herufi hizi ‘Y’, ‘W’, ‘S’, ‘F’, ‘J”, ‘P’, na ‘H’ ni vizuri zaidi. Pendelea sana kumsifu kila utakae kutana nae utaona ajabu.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Wiki hii Bahati itakujia, furaha au barua au habari unazozitarajia utapata, lakini mambo hayo yote yatakuja kwa sharti kwamba lazima upate msaada wa mtu au mkuu fulani au wakili.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Ili kukamilika mipango yako unayotaka lazima ukutane na mtu mmoja mkubwa akiwa yupo hapa au yupo mbali na mkubaliane naye. Utapokutana na huyo mtu lazima umuonyeshe na kumueleza kuwa hali yako ni mbaya na ya wasiwasi. Hata mkikubaliana lazima ujue atakuambia ungoje kidogo au kukucheleweshea mahitaji yako lakini baadae utaokoka.
NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Elewa Katika maisha yako unasaidiwa sana na mtu aliyezaa mtoto wa kiume au baada ya wewe kuzaa mtoto wa kiume utapata bahati nzuri. Unashauriwa kwa ajili ya kufuzu haja yako lazima ufuatane na mtu aliezaa au ufuatane na mtoto wa kiume mdogo utaona ajabu.
MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Katika wiki hii Watu hawa watakusaidia sana:Abi, au Baraka, Bakari au Sadiki. Kwa hiyo kila jambo lako linapokutatiza peleka shauri lako kwa mzee wako Mwanamume.
KAA – CANCER (JUN 22 – JUL 23)
Ukitaka kuoa au kuolewa lazima uoe au uoelewe mtu mwenye umri mdogo chini yako, na mtu ambaye hajaoa au kuolewa. Lazima silaha yako iwe ni kutoa sadaka, shida zako zitakuondokea mara moja. Ukitaka jambo basi tangulia wewe au wewe uwe wa kwanza au ulifanye jambo hilo mbele.
SIMBA – LEO (JUL 24 – AUG 23)
Siku ya leo fikra zako nyingi ni kuhusu ugonjwa au kifungo au mambo yako kuwa mazito na kuharibika haribika, una wasiwasi kwa ajili ya kitu kilichokutoka au mtu aliyekupotea au aliye katika wasiwasi, au kazi kuharibika au wizi.
MASHUKE – VIRGO (AUG 24- SEPT 23)
Siku ya leo Itakubidi ungoje au urejee ulikotoka. Jambo unalodhamiria kulifanya ni bora uliache kabisa na utoe tamaa kwani utalikosa na pana hiyana.Lazima ujue kuwa ukitaka jambo jambo kabla ya wakati wake utapata. majuto kwani utalikosa.
MIZANI – LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Siku ya leo Silaha yako kubwa au njia ya kufanya ni kusubiri na kurudi nyuma na kuacha azimio unalolitaka.Kama una Kesi utashindwa, Mashindano utashindwa, na Mgonjwa yupo hatarini.







0 comments:
Post a Comment