Msanii katika Tasnia
ya Filamu Nchini Kajala Masanja ambaye ni Mzazi mwenzie Produza Pfunk
Majani wa Bongo Records amecharuka na kugeuka Mbogo
kunako Mtandao wa
Instagram kwa kufunguka ya moyoni juu ya Malezi ya Mwanaye Paula
ambaye yeye anaamini kuwa anamlea vizuri na kumfunda maadili
yaliyomema ingawa baadhi ya watu wamekuwa wakifunguka kuwa anamlea
vibaya Mtoto wake huyo ambaye anakuwa kwa Speed ya hatari.
“Nawashangaa sana
watu wengine mnajifanya mnajua sana kuongea kuhusu mambo yasiyo
wahusu kuna mzazi yoyote anataka mwanae apotee ache mambo ya kishamba
unataka mtoto avae dira kwani yeye mtu mzima kama unaona namlea mtoto
wangu vibaya niachie mwenyewe zaa wa kwako mlee vizuri.”







0 comments:
Post a Comment