Mambo yako ya kimapenzi yatakuwa ya
kusuasua sana na migogoro ya mara kwa
mara. Lakini mambo yako ya
kibiashara yatakunyookea sana katika kipindi hiki,Na unatakiwa uwashirikishe ndugu zako ili kupata ufanisi zaidi.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Siku nzuri maisha yako yatakuwa na furaha sana wewe na mpenzi wako au mkeo au mumeo. Mambo yako kikazi yatakunyookea sana na upo uwezekano wa kupandishwa cheo au kuongezwa mshahara.jitayarishe kwa hilo.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Siku ya leo anza kujihusisha na shughuli inayohusiana na pesa kwani kufanya hivyo kutakuletea mafanikio ambayo ulikuwa unayategemea kwa muda mrefu. Biashara za vitu vya maji kama vinywaji na vyakula zitakufaa.
NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Leo kuna mtu ambae atakuletea ugomvi unaotokana na Wivu kwa kukuona umesimama na ndugu yako wa kike.jaribu kumwelea kwa uzuri na jiepushe na maneno makali yanaweza yakakuza ugomvi huo
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
leo hii kuna dalili mbaya hasa ukiwa na shuguli nyingi za kifedha au kibiashara, kwani mambo yako yatakuwa yanakwenda polepole kinyume na ulivyotegemea.kama una mipango mingine ya kifedha ukiachana na hiyo fanya.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Siku ya leo kuna uwezekano wa kushirikishwa katika mazungumzo ya kibiashara ambayo yatakupeleka sehemu nzuri na za kukufurahisha..ukipata nafasi hiyo hakikisha unaikamata kwa nguvu zote.
NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Leo utasumbuliwa sana na watu mbalimbali watakaokujia kutaka msaada au maongezi yasiyo ya kikazi. Kuna habari ya kuvunjika kwa safari yako ya mbali.habari hiyo isikujalishe.
MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Leo ni siku ya mikosi na mabalaa katika nyanja zote. Punguza maneno, majibizano, ugomvi na lolote la mikwaruzano unaweza kupata kesi au kuumia. Jaribu sana kutulia nyumbani kwako unaporudi baada ya shughuli zako za kikazi kuliko kutembea tembea mitaani.
KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Unatakiwa kuwa makini sana katika kipindi hiki cha mpito, kwani kosa dogo tu linaweza kukuleta matatizo.mipango yako uliyokuwa umeipanga na mpenzi wako iahirishe kwa muda wa miezi miwili
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Elewa kuwa kuna mambo mengi ambayo ulikuwa unafichwa na watu wako wa karibu, lakini sasa utayagundua.. Unaonywa kutokufanya makosa na uyaepuke maudhi, hasa kwa mpenzi wako.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Leo unatakiwa kuwa makini na mambo ya mapenzi kwani kosa dogo tu linaweza kusababisha mfarakano mkubwa kati yako na umpendae. Ambae mna mgogoro hivi sasa. Jaribu kupata ushauri wa rafiki yako wa karibu.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo nenda katika shughuli muhimu tu. Shughuli zozote ambazo unaona hazina umuhimu kimapenzi au kimaisha au kipesa jiepushe nazo. Jaribu kuanza mipango mipya uya kimaisha hasa katika mambo ya kipesa.







0 comments:
Post a Comment