Sunday, November 17, 2013

HIKI NDICHO ALICHOANDIKA MWANA FA KWA WALE MABINGWA WA KUTUKANA WATU

Siku zote mtu anapoamua kusema juu ya Jambo fulani hakika huwa amefikia hatua ya juu kabisaa kuchukizwa na Jambo fulani maana katika hali ya kawaida
unaweza kuchuna tu ukiwa na matumaini ya kuwa hayo unayopitia kwa wakati huo ni mapito.

Leo kupitia Mitandao ya Kijamii Msanii Mwana FA amefunguka kuonesha kukereka na baadhi ya watu ambao hutumia Mitandao ya Kijamiii kuwatusi watu wengine,FA amefananisha kitendo hicho kuwa ni sawa na watu hao kukosa kazi za kufanya na kuwa watu hao hawanajitihada za kupigania maisha yao binafsi.

Ukiona una muda wa kuja kwy mitandao ya kijamii kutukana watu,haswa WASIOKUJUA,na hawasumbuki kukujibu na unaendeleza mitusi,ujue huna kazi za kutosha,hupigani sawasawa na maisha yako..get busy,acha utoto...siku njema”

0 comments:

Post a Comment